Mamia ya wanafunzi watoweka Nigeria baada ya shule yao kuvamiwa

Mamia ya wanafunzi wanahofiwa kutoweka baada ya watu waliokuwa na silaha kuvamia shule moja ya sekondari, Kaskazini Magharibi mwa Nigeria.

Wavamizi hao waliwasili kwa pikipiki na kuanza kufyatua risasi hewani, hivyo kusababisha watu kukimbilia usalama wao.

Walioshuhudia kisa hicho wanasema wavamizi hao walilenga shule moja ya Sayansi, iliyo na wanafunzi 800, katika jimbo la Katsina Ijumaa jioni.

Also Read
Rais Lazarus Chakwera akiri kuchangia msambao wa COVID-19 Malawi

Zaidi ya wanafunzi 200 tayari wameokolewa, huku maafisa wa kijeshi na wanahewa wakisema wanashirikiana kuwatafuta wale waliotoweka.

Majirani wa shule hiyo ya wavulana katika eneo la Kankara wamewaambia waandishi wa habari kwamba walisikia milio ya bunduki mwendo wa saa tano usiku wa Ijumaa, na kwamba uvamizi huo ulichukua zaidi ya saa nzima.

Also Read
Marekani kuwaondoa wafanyikazi wake katika ubalozi wa Kabul

Maafisa wa usalama kwenye shule hiyo walifanikiwa kuwatimua baadhi ya wavamizi kabla ya polisi kufika.

Also Read
Mercy Johnson apendeza kwenye hafla ya kuwekwa wakfu kwa mtoto wake

Taarifa ya polisi inasema wakati wa makabiliano ya risasi, baadhi ya wavamizi walilazimika kurudi nyuma na kwamba wanafunzi waliweza kuruka ua wa shule yao na kukimbilia usalama.

Hata hivyo, mashahidi wa kisa hicho wanasema waliwaona wavamizi hao wakiondoka na baadhi ya wanafunzi.

  

Latest posts

Shule nchini Uganda kufunguliwa Januari mwaka 2022

Tom Mathinji

Mgomo wa wahudumu wa afya wasababisha maafa Guinea Bissau

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika azikwa Jijini Algiers

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi