Manara na Hersi Matatani

Kamati ya maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewafungulia mashtaka Rais wa Yanga mhandisi Hersi Said na aliyekuwa afisa wa mawasiliano wa klabu hiyo Haji Manara kwa kukiuka sheria. Manara alihusika na sherehe ya siku ya wananchi almaarufu Yanga Day jana Jumamosi tarehe 6 mwezi Agosti mwaka 2022. Akiwa huko alitambulisha wachezaji wapya ambao timu hiyo imesajili kwa ajili ya msimu mpya.

Also Read
Real Madrid na PSg kuvaana EUFA Champions league

Mwezi jana, kamati hiyo ya Maadili ya TFF ilimfungia Manara kwa miaka miwili na katika muda huo hatakiwi kujihusisha na shughuli zozote za mpira wa miguu nchini Tanzania. Kosa lililosababisha adhabu hiyo kwa Manara ni maneno aliyomwambia rais wa shirikisho la soka nchini Tanzania Wallace Karia tarehe 2 mwezi Julai mwaka huu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid katika eneo la kukaribishia wageni mashuhuri. Manara anasemekana kumzomea Karia akisema amekuwa akimfuatafuata sana na kwamba hiyo ilikuwa mara ya tatu isijulikane walichokuwa wakizozania. Baada ya vikao vya kusikiliza kesi iliyowasilishwa na Karia, Manara alikana makosa lakini ikabainika kwamba alikuwa na hatia.

Also Read
Walinda usalama wawili wa Umoja wa Mataifa wauawa nchini Mali
Also Read
Kikosi cha Shujaa kwa michezo ya jumuiya ya madola chatajwa

Mhandisi Said naye amejipata pabaya baada ya kukosa kutekeleza agizo la TFF. Baada ya Manara kupigwa marufuku kwa muda wa miaka miwili, TFF ilimwandikia waraka mhandisi Hersi Said kumwelekeza ahakikishe kwamba Manara hajihusishi na soka kwa vyovyote.

  

Latest posts

Kipchoge na Kipruto warejea nyumbani kutoka London

Dismas Otuke

Gonzalo Higuain astaafu rasmi kutoka soka

Dismas Otuke

Takwimu za kipute cha 22 cha kombe la dunia nchini Qatar

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi