Maombolezo ya Diop yaendelea

Risala za rambi rambi zingali zinamiminika kumwomboleza mchezaji nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Senegal Papa Bouba Diop aliyeaga dunia Jumapili usiku  akiwa na umri wa miaka 42 kwa mjibu wa taarifa kutoka shirikisho la kandanda nchini Senegal FSF .

Shirikisho la kandanda ulimwenguni Fifa limeongoza risala hizo likisema limesikitishwa na kifo cha mwanandinga huyo .

Mshambulizi wa Uingereza  Ademola Lukman pia alikuwa na jezi ya Senegal iliyokuwa ikivaliwa na marehemu Diop  na kuibeba punde baada ya kufunga bao Jumatatu usiku alipoisaidia timu yake ya Fulham kuichapa Leicester City mabao 2-1 katika ligi kuu Uingereza.

Also Read
Rwanda Uganda waumiza nyasi bila lengo
Lukman akiinua jezi ya Senegal nambari 19 iliyokuwa ikivaliwa na Diop punde baada ya kufunga bao Jumatatu usiku

Diop aliichezea timu ya taifa ya Senegal maarufu kama Teranga Lions mechi 63 huku akigonga vichwa vya habri alipofunga bao la pekee wakati timu hiyo ikiwaduwaza mabingwa wa dunia Ufaransa kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 2002.

Baadae katika fainali hizo kombe la dunia mwaka 2002 huko Korea Kusini na Japan marehemu alipachika kimiani mabao 2 zaidi  huku wakicheza hadi robo fainali kwa mara ya kwanza .

Also Read
AFCON kuandaliwa baina ya Januari 9 na Februari 6 mwaka ujao nchini Cameroon
Diop baada ya kufunga bao mwaka 2002 kdhidi ya Ufaransa

Diop alizichezea timu za Uingereza Fulham na Portsmouth na alikuwa katika timu ya Portsmouth iliyonyakua kombe la FA mwaka 2008.

Diop alizaliwa mjini Dakar Senegal Januari 28 mwaka 78 na alianza kusakata soka mwaka 1994  na kilabu ya Difan Saltique nchini Senega,l kabla ya kujiunga na Asc Diaraf  ya Senegal mwaka 1996 na kuelekea Uswizi alikopiga na kilabu cha Vevey United  mwaka 1999  kisha akahamia Nuchatel Xamax ya  Uswizi mwaka 2000.

Also Read
Gor wawashika mateka wanajeshi wa Rwanda APR na kufuzu kwa mchujo wa pili

Bouba alijiunga na  Grasshoppers ya Uswizi mwaka 2001,kabla ya kuhamia Lens mwaka 2002 na kutua Fulham mwaka 2004 hadi 2007 kisha akatua  Portsmouth  kati ya mwaka 2007  na  2010 na kuhama tena hadi Ugiriki maka 2010 akiwa na Aek Athens.

Kiungo huyo mkabaji alirejea tena Uingereza mwaka 2011-2012 akiipigia Westham United kabla ya kustaafu akiwa Birmingham City mwaka  2013 akisakata jumla ya michuano 261 na kupachika mabao 26 na mechi 63 akiwa na  timu ya taifa kati ya mwaka 2001 na 2008 akifunga mabao 11.

 

 

 

  

Latest posts

Elain Thompson awaongoza vidosho wa Jamaica kufagia medali zote za mita 100

Dismas Otuke

Kenya yaambulia pakavu baada ya Moraa kukosa kufuzu kwa fainali ya ita 800 vipusa

Dismas Otuke

Omanyala Omurwa afuzu kwa nusu fainali ya mita 100 Olimpiki na kusawazisha rekodi ya kitaifa

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi