Maraga asifu mfumo wa dijitali wa shughuli za mahakama

Jaji Mkuu David Maraga amekariri umuhimu wa kutekeleza shughuli za mahakama kwa njia ya dijitali ili kurahisisha shughuli ya kutafuta faili za kesi.

Maraga ametaja uhifadhi wa kumbukumbu kuwa moja ya changamoto zinazoshuhudiwa katika utekelezaji wa haki.

Amesema mfumo huo wa dijitali utawezesha wanaotafuta haki kupata faili za kesi za kuanzia miaka ya 1950 zinazohifadhiwa kwenye mabohari ya mahakama.

Also Read
Idara ya Mahakama yaondolewa kizuizi cha uteuzi wa Jaji Mkuu

“Tukiwa na teknolojia hizo faili itakuwa rahisi sana kuzipata, hata kama ni miaka 20 au 50 kwa hivyo tusaidiane tuende kwa teknolojia,” amesema Maraga.

Also Read
Rais Kenyatta amtaja marehemu John Magufuli kuwa mzalendo wa kuigwa

Akizindua mahakama mpya katika makao makuu ya Kaunti Ndogo ya Borabu Kaunti ya Nyamira, Jaji Mkuu aliwahimiza wakazi wazingatie njia mbadala ya utatuzi wa mizozo kwa njia ya upatanishi akisema ndio mfumo bora wa kushughulikia mizozo hasa inayohusu masuala ya urithi.

Also Read
Wakili Fred Ngatia asailiwa na jopo la JSC, kuwania wadhifa wa Jaji Mkuu

Maraga amesema mfumo huo mbadala unahakikisha pande husika zinaafikia suluhu mwafaka na kudumisha mahusiano yao.

Jaji Mkuu amewahimiza machifu wasaidie mahakama katika kubaini watu halisi wanaofaa kunufaika katika mizozo ya ardhi kwa kuelewa asili za familia.

  

Latest posts

Visa 394 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Chris Obure ana kesi ya kujibu kuhusiana na sakata ya Anglo Leasing

Tom Mathinji

Rais Kenyatta atoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa Kilimo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi