Marefa wa Kenya Mary Njoroge na Gilbert Cheruiyot kusimamia soka ya Olimpiki

Waamuzi wa kenya Mary Njoroge na Gilbert Cheruiyot wameteuliwa kusimamia mechi za soka katika michezo ya Olimpiki mwaka huu mjini Tokyo Japan baina ya Julai 23 na Agosti 8.

Itakuwa mara ya kwanza kwa Mary Njoroge kusimamia soka katika kiwango  hicho ,baada ya kusimamia mechi za kombe la dunia kwa wanawake mwaka 2019,kusimamia mechi moja  hatua ya makundi kuwania kombe la shirikisho baina ya vilabu,mechi moja ya kufuzu kwa kombe la AFCON mwaka ujao kando na kuwa mwamuzi katika mechi kadhaa za ligi kuu Kenya FKF msimu huu.

Also Read
Majaribio ya kitaifa kuchagua timu ya vijana wasiozidi umri wa miaka 20 yaanza Kasarani
Refarii Mary njoroge akifanya mazoezi

Njoroge atakuwa mwamuzi wa mechi za soka za wanawake nchini Japan.

Also Read
Onyango kucheza hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika kwa mara ya kwanza

Kwa upande wake Cheruiyot alisimamia mchuano wa kwota fainali kuwania  kombe la CHAN ,kando na kuwa mwamuzi msaidizi katika mechi ya kufuzu kwa  kombe la AFCON baina ya Ethiopia na Ivory Coast pia amekuwa akisimamia mechi za ligi kuu FKF.

Also Read
Japan yatangaza hali ya hatari kutokana na Covid 19 Miezi mitatu kabla ya kuanza kwa Olimpiki

Wawili hao wameteuliwa kuwa marefarii wasaidizi katika michezo ya Olimpiki  ambayo itasimamiwa na marefarii 25  na wasiaidizi 50  pamoja na waamuzi 20 VAR  kutoka mataifa 51.

Soka ya akina dada katika michezo ya Olimpiki itang’oa nanga Julai 21 huku ile ya wanaume ikianza Julai 22

 

  

Latest posts

Police Fc washerehekea kurejea ligi kuu baada ya mwongo mmoja kwa dhifa

Dismas Otuke

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Vidosho wa Kenya wapigwa dafrao na Msumbiji mashindano ya kikapu Afrika

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi