Marekani yaahidi kuunga mkono juhudi za kenya za kudumisha amani

Rais wa Marekani Joe Biden ametaja umuhimu wa ushirikiano dhabiti kati ya Kenya na Marekani huku akitoa ahadi kuwa ataendelea kuunga mkono ushirikiano huo. 

Katika mazungumzo kupitia njia ya simu kati ya rais huyo wa Marekani na Rais Uhuru Kenyatta Alhamisi jioni, Rais Biden alisifia kujitolea kwa Kenya kudumisha amani na usalama katika kanda hii na kuahidi kushirikiana na nchi hii katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kulinda udhabiti wa kanda hii. 

Miongoni mwa masuala waliyozungumzia ni pamoja na uhusiano kati ya Kenya na Marekani, uchumi, usalama na amani, mabadiliko ya hali ya hewa na haki za binadamu.

Aidha, Biden aliipongeza Kenya kwa kujitolea kwake kupiga vita ugaidi, kuimarisha uchumi wa taifa na kuangazia masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa na maendeleo endelevu katika eneo la upembe wa Afrika.

Kwa upande wake, Rais Uhuru Kenyatta, alieleza matumaini ya kukamilishwa kwa haraka mashauriano yanayoendelea kuhusu biashara huru kati ya Kenya na Marekani.

Kenya imeorodheshwa ya nne bora miongoni mwa mataifa yanayoshirikiana kibiashara na Marekani barani Afrika.

Kwa mara nyingine Rais Kenyatta alimshukuru mwenzake wa Marekani kutokana na msaada wake kwa taifa hili hasaa katika sekta ya Afya,uchumi, Usalama na uongozi. Alimhakikishia Rais Biden kujitolea kwa kenya kufanya kazi kwa karibu na utawala mpya wa Marekani,” alisema Kanze Dena ambaye ni msemaji wa Ikulu.

  

Latest posts

Rashid Aman: Chanjo zinazotolewa hapa nchini ni salama

Tom Mathinji

Kampuni ya sukari ya Nzoia yalaumiwa kwa kutowalipa wakulima

Tom Mathinji

China kupiga jeki uwezo wa kuzalisha chanjo hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi