Marekani yagomea uchaguzi mkuu wa Uganda

Marekani haitashiriki katika uangalizi wa uchaguzi mkuu wa Alhamisi nchini Uganda.

Hii ni kutokana na hatua ya tume ya uchaguzi nchini humo kukataa asilimia 75 ya maombi ya Marekani ya kuwapa idhini waangalizi ili kushiriki katika uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa Balozi wa Marekani nchini Uganda Natalie Brown, tume hiyo haikutoa maelezo kuhusiana na uamuzi huo, licha ya kuwasilishwa kwa maombi kadhaa.

Also Read
Mwanamke anayedaiwa kuiba kompyuta ya Spika Pelosi Marekani atiwa nguvuni

Amesema kuwa ni waangalizi wachache tu ndio walioteuliwa kutoka kwa kundi la watu 88.

Ameongeza kuwa uchaguzi huo mkuu wa Uganda utakosa uwazi na imani ambayo hutokana na kuwepo kwa waangalizi kutoka mataifa ya nje.

Raia wa Uganda watawachagua wabunge wapya na rais katika uchaguzi huo wa Alhamisi.

Also Read
Shinikizo la Rais Xi kuhusu juhudi za pamoja za kupambana na covid-19 lazaa matunda
Also Read
Mwanafunzi raia wa Cameroon ashtakiwa Marekani kwa utapeli

Rais Yoweri Museveni, ambaye amekuwa mamlakani kwa miaka 35, atakuwa akiwania muhula wa sita mamlakani.

Hata hivyo Museveni anatarajiwa kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mgombea wa upande wa upinzani Bobi Wine.

  

Latest posts

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amefariki

Tom Mathinji

Ethiopia yakaribisha wito wa kurejelewa mazungumzo na majirani wake kuhusu bwawa katika mto Nile

Tom Mathinji

Bwawa katika mto Nile lazidisha uhasama kati ya Ethiopia, Sudan na Misri

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi