Mark Otieno aondolewa Olimpiki Tokyo kwa ulaji muku

Mwanariadha wa Kenya Mark Otieno ameondolewa kushiriki mchujo wa mita 100 katika michezo ya Olimpiki baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa za kututumua misuli.

Otieno anayeshiriki Olimpiki kwa mara ya kwanza alikuwa ashiriki mchujo wa mita 100 kuanzia saa saba adhuhuri ya Jumamosi .

Also Read
Washukiwa wawili wa mauaji ya Herman Rouwenhourst kuzuiliwa kwa siku 21 zaidi

Taarifa hii ina maana kuwa ni Ferdinand Omanyala pekee atakayeshiriki mchujo huo.

Mark Otieno

Kulingana  na taarifa kutoka kwa kingozi wa ujumbe wa Kenya  katika michezo ya Olimpiki ,Waithaka Kioni sampuli ya mkojo iliyochukuliwa kutoka kwa mwanariadha huyo tarehe 28 mwezi uliopita imeashirikia ametumia dawa za kututumua misuli.

Also Read
Wanariadha waliokuwa kambi Embu kuathiriwa na kuahirishwa kwa mashindano ya Afrika ya mbio za Nyika

Hata hivyo Otieno amekanusha kutumia dawa yoyote ya  kuongeza nguvu mwilini na kuomba uchunguzi wa pili ufanywe.

Otieno ni mwanariadha wa kwanza wa Kenya  kupatikana kuwa mtumizi wa dawa zilizoharamishwa katika michezo ya Olimpiki inayoendelea.

Also Read
Musalia Mudavadi: Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2022 haupaswi kuahirishwa

Mapema leo kitengo cha maadili ya wanariadha AIU kimempiga  marufuku Blessing Okagbare  wa Nigeria kwa kupatikana na hatia ya kutumia dawa zilizoharamishwa michezoni.

 

  

Latest posts

Idadi ndogo ya wakazi wa Nairobi wajitokeza kuchanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Omanyala aweka rekodi mpya ya Afrika ya mita 100 ya sekunde 9 nukta 77 Kip Keino Classic

Dismas Otuke

Watumishi wa Umma wahimizwa kushirikisha taasisi mbali mbali kufanikisha majukumu yao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi