Gavana wa Embu Martin Wambora amechaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa baraza la Magavana bila kupingwa.
Gavana wa Kisii Jame Ongwae, na mwenzake wa Elgeyo Marakwet Alex Tolgos, wataendelea na wadhifa wao wa naibu mwenyekiti na kiranja wa baraza hilo mtawalia.
Katika hotuba yake, Wambora alisema ataendelea kutoa mwongozo kwa baraza hilo Licha ya kuwepo kwa changamoto za janga la COVID-19.
“Ninafuraha kwa hatua ya wenzangu ya kuwa na Imani kwangu. Ni heshima kubwa kutoa uongozi na mwelekeo kwa muhula mwingine,” alisema Wambora.
Uchaguzi huo uliandaliwa katika hoteli moja Jijini Nairobi, na kuhudhuriwa na Magavana wote 47.
Mwenyekiti wa kwanza wa baraza la Magavana nchini alikuwa Gavana wa zamani wa Bomet Isaac Ruto na Kisha aliyekuwa Gavana wa Meru Peter Munya akachukua usukani.
Gavana Wambora alichukua hatamu za uongozi mwezi Januari mwaka 2021.