Marufuku ya Kenya ya kuuza maembe Ulaya kuondolewa Septemba

Kenya itaondolewa marufuku ya miaka saba ya uuzaji maembe Barani Ulaya mnamo mwezi Septemba mwaka huu.

Hii ni baada ya serikali kushughulikia masuala yaliyosababisha maembe ya Kenya kupigwa marufuku katika masoko hayo kutokana na wasi wasi kuwa yana wadudu waharibifu.

Also Read
Kongamano kuhusu ugatuzi laahirishwa

Marufuku hiyo ilianza kutekelezwa mwaka wa 2014, kutokana na ukosefu wa ubora kwenye maembe ya Kenya.

Also Read
Benki ya family yatoa vifaa vya matibabu vya shilingi milioni moja kwa kaunti ya Makueni

Wauzaji watatu wa maembe kutoka Kaunti ya Makueni tayari wameidhinishwa kuanza kusafirisha maembe yao Barani Ulaya baada ya Kenya kudhibiti wadudu hao.

Also Read
Serikali ya Kaunti ya Kilifi yakabidhiwa usimamizi wa kiwanda cha sharubati huko Malindi

Wakulima wa mazao ya maembe wameshauriwa kukuza aina ya maembe yanayokua kwa haraka.

Mwaka uliopita, Kenya iliuza jumla ya tani 11 za maembe katika eneo la Mashariki na Kati.

  

Latest posts

Wakazi wa Nandi ya kati wahimizwa kushirikiana na polisi kukabiliana na uhalifu

Tom Mathinji

Serikali yahimizwa kutoa mikopo ya HELB kwa wanafunzi wa vyuo vya kibinafsi

Tom Mathinji

Mahakama iko tayari kwa kesi za uchaguzi mkuu ujao asema Jaji mkuu Martha Koome

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi