Mary Moraa Bingwa wa Mita 800 kwa Wanawake Kwenye Michezo ya Jumuia ya Madola Mwaka 2022

Mwanariadha wa Kenya Mary Moraa ndiye bingwa wa mbio za mita 800 kwa upande wa kina dada kwenye michezo ya Jumuia ya Madola mwaka 2022. Moraa alishinda nishani ya dhahabu kwenye mbio hizo kwa muda wa dakika moja na sekunde 57.07 mbele ya mwingereza Keely Hodgkinson aliyetumia muda wa dakika moja na sekunde 57.40.

Also Read
Moraa alenga ushindi Kip Keino Classic

Laura Muir mwanariada wa nchi ya Scotland alijikaza na kunyakua nishani ya shaba mbele ya Natayo Goule wa Jamaica. Muir aliandikisha muda wa dakika moja na sekunde 57.87 na Goule akakimbia kwa dakika moja sekunde 57.88.

Also Read
Shujaa yabanduliwa nje ya nishani baada ya kupigwa kitutu na Newzealand michezo ya jumuiya ya madola
Also Read
Moraa awaangusha vigogo na kufuzu kwa Olimpiki

Ushindi wa Mary Moraa unajiri siku chache baada yake kunyakua nishani ya shaba kwenye mbio sawia katika mashindano ya riadha ya dunia jijini Oregon nchini Marekani.

  

Latest posts

Wetangula kuamua Alhamisi ni chama kipi kitashikilia wadhifa wa kiongozi wa wengi bungeni

Tom Mathinji

Kipchoge na Kipruto warejea nyumbani kutoka London

Dismas Otuke

Rais William Ruto ampokea Mpambe mpya

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi