Mashabiki 10,000 kuingia Nyayo kwa mechi ya Gor Mahia dhidi ya Otoho Jumapili

Mashabiki wasiozidi 10,000 wameruhusiwa kuingia uwanja wa kitaifa wa Nyayo kushuhudia mchuano wa marudio ,mchujo wa pili kuwania kombe la shirikisho Afrika baina ya Gor Mahia na AS Otoho D Oyo ya Congo Brazzaville.

Kupitia kwa ukurasa twitter wa klabu ya Gor Mahia, tiketi za kuingia uwanjani Nyayo zinauzwa kwa shilingi 500 kwa zile za VIP na shilingi 200 kwa tiketi za maeneo ya kawaida, huku shughuli ya kuuza tiketi ikifunguliwa rasmi Jumapili kuanzia saa mbili asubuhi.

Also Read
Ligi ya mabingwa Afrika kwa wanawake kuanza Ijumaa Cairo

Itakuwa mara ya kwanza kwa mashabiki kuruhusiwa kuingia uwanjani kwa mchuano wa Gor Mahia tangu mwaka 2019 .

Also Read
Mkufunzi wa makipa wa Gor Mahia Willis Ochieng ajiuzulu

Gor Maarufu kama Kogalo ambao walirejea mazoezinini Jumatano,watalazikika kusajili ushindi wa mabao 2-0 ili kutinga hatua ya makundi ya kombe hilo baada ya kaumbulia kichapo cha bao 1-0 ktika duru ya kwanza Jumapili iliyopita.

Also Read
Omanyala aanza mashindano ya Afrika kwa kishindo

Mabingwa hao mara 20 wa Kenya ambao wanakumbwa na uhaba wa wachezaji wamepata afueni baada ya wanandinga mshambulizi Jules Ulimwengu na beki John Ochieng kuwasili nchini Kenya Alhamisi kutoka Brazzaville walikozuliwa baada ya kupatikana na virusi vya Covid 19.

  

Latest posts

Japhet Koome ateuliwa Inspekta Jenerali wa Polisi

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi ateuliwa waziri mwenye Mamlaka zaidi

Tom Mathinji

Wanawake saba wateuliwa katika baraza jipya la Mawaziri

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi