Mashabiki kuingia Kip Keino classic uwanjani Kasarani bila malipo

Mashabiki wataruhusiwa kuingia uwanja wa kimataifa wa Kasarani Jumamosi kushuhudia makala ya tatu ya mashindano ya Kip Keino Classic continental tour bila malipo baada ya wizara ya michezo kufutilia mbali ada iliyokuwa imewekwa kama kiingilio na waandalizi.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari Ijumaa ,waziri wa Michezo Dkt Amina Mohammed ametangaza kuwa wameondoa ada hiyo,ili kuwaruhusu Wakenya wengi kufika uwanjani kushuhudia mashindano .

“Ili kuwaruhusu mashabiki wengi kuja uwanjani kushuhudia mashindano tumeondoa malipo ,na tunawataka watu waje kwa wingi kuwashangilia wanariadha wa nyumbani”akasema Amina

Also Read
Mashindano ya dunia riadha ya viwanja vya ndani yaahirishwa hadi 2023

Mashindano hayo yatashuhudia wanariadha 160 wa kutoka humu nchini na wale wa kimataifa wakishindana katika vitengo vitatu vya Kitaifa,discretionary na kitengo kikuu cha Core Events ambacho ni cha kuwania pointi pamoja na zawadi ya pesa .

Kip Keino Classic ni mashindano ya mzunguko wa tatu katika mashindano ya nenmbo ya dhahabu baada ya Bermuda tarehe 9 mwezi jana na yale ya Marekani tarehe 16 mwezi April.

Also Read
Limbukeni Uganda Hippos yaivyoga Tunisia na kutinga fainali ya AFCON 20

Mashindano yanayotarajiwa kuwa na msisimko ni mita 3000 kuruka viunzi na maji ambapo bingwa wa Olimpiki Peruth Chemutai wa Uganda atakabiliana na bingwa mtetezi Celphine Chespol.

Pia katika mita 100 wanaume bingwa wa Olimpiki Marcel Jacobs kutoka Italia na mshindi wa nishani ya fedha ya Olimpiki Fred Kerley wa Marekani watakabiliana na mshikilizi wa rekodi ya Afrika Ferdinand Omanyala kuanzia saa kumi na mbili jioni.

Also Read
Mshikilizi wa zamani wa rekodi ya dunia ya marathon Paula Radcliff atua Kenya

Fainali ya mita 100 wanawake pia itashuhudia mshindi wa nishani ya fedha ya Olimpiki katika mita 200 Christine Mboma wa Namibia akipimana nguvu na bingwa mara tatu wa Olimpiki Shell Ann Fraser Pryce kutoka Jamaica.

Awali waandalizi walikuwa wametangaza kuwa mashabiki wangelipa ada ya shilingi 200 kwa maeneo ya kawaida na shilingi 1500 kwa eneo la VIP .

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi