Mashabiki wa Diamond Platinumz walalamikia muda kidogo alipatiwa kwenye wimbo wa Alicia Keys

Mashabiki wa Diamond Platinumz walionyesha kutoridhika na muda kidogo ambao Diamond alipatiwa kwenye wimbo wa mwanamuziki wa Marekani Alicia Keys. 

Kwenye wimbo huo kwa jina “wasted energy” Diamond ameimba kwa sekunde 26 pekee! Kunako dakika ya tatu sekunde ya 35 ndio Diamond anaingia ilhali wimbo ni dakika nne sekunde 10.

“Kwa nini penzi umelikata miguu, unalibidua mara chini mara juu, Why? why? Moyo unaumia, moyo unaumia, moyo unaumia, kwa nini unageuza nguo karaha? Eti Karaha oh, oh” Ndiyo maneno Diamond ameimba mwishoni mwa “wasted energy”.

Album hiyo mpya ya Alicia Keys kwa jina “Alicia” ilizinduliwa ijumaa tarehe 18 mwezi Septemba mwak 2020 baada ya kusubiriwa kwa hamu na ghamu.

 

Also Read
Vituko vya Eric Omondi
Alicia Keys

 

Also Read
Gari La Tupac Shakur Linauzwa

Mashabiki hao walitumia mitandao ya kijamii kuonyesha kutoridhika na muda mchache ambao nyota wao alipatiwa na mmarekani Alicia. Lalama hizo zilimfikia mtayarishaji muziki kwa jina Swizz Beats ambaye pia ni mume wa Alicia Keys.

Swizz alimhimiza Diamond awakanye mashabiki wake na awaeleze kwamba ni yeye alitaka hivyo na kwamba ni mwanzo tu wa kazi nyingi za pamoja kimziki.

“Simba” anavyojiita Diamond aliandika kwenye instagram akiridhia maelezo ya Swizz.

Mwezi wa pili mwaka huu Diamond alikuwa mwanamuziki ambaye kazi zake zilipata kutazamwa na watu wengi zaidi kwenye Youtube, eneo la Afrika Mashariki.

Wimbo ambao ulikuwa umetazamwa sana ni ule uitwao “yope remix” ambapo Innos B wa Congo alimshirikisha.

  

Latest posts

Hata Nikifa Wanangu Hawatateseka – Asema Akothee

Marion Bosire

Miaka 70 ya Uwepo wa Ukumbi wa Maonyesho ya Sanaa

Marion Bosire

Ringtone Atangaza Kwamba Ameacha Kuimba Nyimbo za Injili

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi