Mashemeji wasusia Derby ya Jumamosi hadi FKF itoe posho ya Milioni 3

Gor Mahia na AFC Leopards wamesusia derby ya Jumamosi ya ligi kuu kuteta hatua ya shirikisho kuchelewesha kuwalipa kima cha shilingi milioni 3 walizostahili   kutuzwa baada  ya kucheza fainali ya kombe la FKF lililofadhiliwa na kampuni ya kamari ya Betway.

Also Read
Mkondo wa nne wa Continental tour wa Ostrava Golden Spike kuandaliwa Jumatano

Kulingana na barua ya pamoja iliyoandikwa na kusainiwa na wenyeviti wawili wa vlabu hiyo Dan Shikanda wa Leopards na Ambrose Rachier wa Gor Mahia  timu hizo zimesema hazitacheza mchuano huo hadi walipwe pesa hizo ,Gor wakistahili kulipwa shilingi milioni 2 kwa kuibuka mabingwa wa kombe hilo wakati  Ingwe wakidai milioni 1 kwa kumaliza katika nafasi ya pili.

Also Read
Mashindano ya Africa kufuzu kwa Olimpiki katika Beach Volleyball kuandaliwa Juni

Timu hizo kwa sasa zinakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi kufuatia hatua wafadhili wao kampuni ya Betsafe kutangaza kupunguza ufadhili wao kuanzia Julai Mosi mwaka huu kufuatia kupitishwa kwa sheria mpya ya kuongeza ushuru wa kamari.

Also Read
Niyonsaba avunja rekodi ya dunia ya mita 2000 Zagreb

 

 

  

Latest posts

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Vidosho wa Kenya wapigwa dafrao na Msumbiji mashindano ya kikapu Afrika

Dismas Otuke

FKF yakatiza mkataba wa shilingi milioni 127 na Odibets

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi