Mashindano ya dunia riadha ya viwanja vya ndani yaahirishwa hadi 2023

Shirikisho la riadha ulimwenguni limetangaza  kuahirisha mashindano ya dunia ya viwanja vya ndani maarufu kama World Athletics Indoor Championships.

Kwa mjibu wa waandalizi wa mashindano hayo  yaliyopaswa kuandaliwa mjini Nanjing China kati ya Machi 19 na 21 mwaka ujao   mashindano hayo yameahirishwa hadi  mwezi Machi mwaka 2023.

Also Read
Ingwe yaichuna Sharks huku KCB wakiwazima Western Stima

Kulingana na kamati andalizi ya mashindano hayo ,wamelazimika kuchukua hatua hiyo kutokana na janga la Covid 19 ambalo bado limtenda kote ulimwenguni na hakuna dalili za ugonjwa huo kudhibitiwa ifikiapo mapema mwaka ujao ili kuruhusu mashindano hayo kuandaliwa mwezi Machi mwakani.

Also Read
Kandie aweka rekodi mpya ya dunia ya nusu marathon Valencia

Imekuwa vigumu kuhamisha mashindano hayo kutoka mwezi Machi hadi baade mwaka ujao kutokana na kalenda fupi ya mashindano ya indoors.

Mashindano hayo ambayo ni ya makala ya 18 yaliratibiwa kuandaliwa baina ya Machi 15-18 mwaka huu kabla ya kusukumwa mbele hadi mwaka 2021 na sasa yameahirishwa tena hadi mwaka 2023.

Also Read
Safari ya kwenda Qatar 2022 yaanzia Amerika Kusini

Kenya ilinyakua nishani moja pekee ya shaba ya mita 3000 katika makala ya mwaka 2018 mjini Birmingham Uingereza.

 

 

  

Latest posts

Tusker ,Gor Mahia kufungua pazia kwa mechi ya Super Cup Jumatano

Dismas Otuke

Vidosho wa Kenya kutoana jasho na Senegal Jumatano kusaka tiketi ya kwota fainali FIBA Afrobasket

Dismas Otuke

Shujaa yaangukia kundi moja na Uhispania,USA na Chile mkondo wa Edmonton 7’s

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi