Mashirika ya kidini yatakiwa kusaidia katika upanzi wa miti

Serikali imetoa wito kwa mashirika ya kidini kutumia raslimali nyingi walizonazo kusaidia kuongeza kiasi cha misitu nchini kutoka asilimia 7.2% hadi 10% kufikia mwaka wa 2022.

Kupitia wizara ya mazingira, serikali inataka ushirikiano na mashirika ya kidini kusaidia katika shughuli inayoendelea ya kupanda miti.

Also Read
Serikali yajizatiti kuhakikisha inaafikia kiwango cha asilimia 10 ya misitu nchini

Akiongea baada ya kukutana na wawakilishi wa baraza la mashirika ya kidini , katibu katika wizara ya mazingira Dkt Chris Kiptoo alitaka mashirika hayo kutumia ardhi wanayomiliki kukuza miche.

Also Read
Kenya yaungana na mataifa ya Afrika kwenye azimio la utunzi wa mazingira

Dkt Kiptoo pia aliwataka viongozi wa kidini kuwashauri wafuazi wao kushiriki kwenye shughuli za kupanda miti.

Askofu Joseph Mutie, kutoka baraza hilo aliunga mkono wito wa ushirikiano huo. Naibu mkurugenzi wa taasisi ya idara ya misitu Dr. Jane Njuguna, amesema taasisi hiyo itatoa mwongozo wa jinsi ya kukuza miche ili ifikie bilioni 1.8 inayohitajika.

  

Latest posts

John Nkengasong: Omicron sio virusi vipya vya Covid-19

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi milioni 2 za chanjo aina ya AstraZeneca kutoka Ujerumani

Tom Mathinji

Watu 96 zaidi waambukizwa COVID-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi