Mashirika yakuwatafutia watu kazi yanayokiuka sheria yaonywa

Wizara ya leba na maslahi ya jamii imeonya mashirika ya kuwatafutia watu nafasi za ajira yanayotekeleza shughuli zao nchini kinyume cha sheria kwamba huenda zikashtakiwa na biashara zao kufungwa.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa kamati kuhusu kuratibiwa kwa mikakati ya usimamizi na maoni ya jamii jijini Nairobi, waziri Simon Chelugui alisema kuwa ni asilimia 40 pekee ya mashirika hayo yametii sheria.

Also Read
Mwanaume aliyewabaka bintize ahukumiwa miaka 140 gerezani

Chelugui alisema kuwa wizara hiyo iemanzisha msako dhidi ya mashirika haramu.

Also Read
Wanafunzi 99 wameambukizwa Corona tangu kufunguliwa kwa shule kaunti ya Siaya

Alisema kuwa wizara hiyo imebuni mikakati ya kuhakikisha kwamba mashirika yote yanasailiwa ili kutii viwango vya maadili.

Chelugui alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kukomesha kupunjwa na kudhulumiwa kwa wakenya wanaofanya kazi katika nchi za ng’ambo.

Also Read
Rasi wa Tanzania Samia Suluhu kuzuru Kenya Jumanne

Chelugui aliongeza kusema kuwa wizara hiyo inaratibu mpango wa kuongeza idadi ya wakenya wanaofanya kazi nje, akisema kuwa kiasi cha pesa zinazotumwa na wakenya kutoka nje kimekuwa kikiongezeka.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi