Masomo yarejelewa Laikipia huku usalama ukiimarishwa

Usalama uliimarishwa katika eneo la Ol-Moran, kaunti ya Laikipia, huku wanafunzi na waalimu wakianza kurejelea masomo kufuatia agizo la serikali.

Uchunguzi uliofanywa na shirika la KBC ulionyesha kuwepo kwa idadi ndogo ya wanafunzi kwenye shule zinazohusika.

Katika shule ya msingi ya Ol-Moran, wanafunzi 65 pekee kati ya 582 ndio walikuwa wamefika shuleni.

Also Read
Shule yajengwa kuleta amani, Samburu,Laikipia na Pokot

Kulingana na mwalimu mkuu wa shule hiyo James Tinega, wazazi wengi bado wana hofu ya kurejea katika makaazi yao.

Na katika shule jirani ya Tumaini Academy, wasimamizi walihamisha wanafunzi hadi uwanja wa kanisa katoliki. Msiammizi wa shule hiyo Peterson Muthua alisema shule hiyo imejengwa msituni, na hivyo imekuwa vigumu kushawishi wanafunzi na wazazi kurejelea amsomo.

Also Read
Wito watolewa wa kurejeshwa kwa polisi wa akiba Laikipia

Na katika shule ya msingi ya Miharati, wanafunzi na waalimu hawakufika shuleni, ilhali ni wanafunzi wawili pekee waliojitokeza kwenye shule ya msingi ya Mirigwet.

Also Read
Raila Odinga: Kenya inahitaji viongozi watakaounganisha nchi hii

Wakati huo huo; Mshirikishi wa eneo la Rift-Valley George Natembeya amehimzia raia kurejea katika makaazi yao, akisema mipango ya usambazaji chakula itapelekwa mashinani

  

Latest posts

Nyongeza ya bei za mafuta yapingwa Mahakamani

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa 113 vipya vya COVID-19

Tom Mathinji

Wazazi wasema watatetea mtaala mpya wa Elimu wa CBC

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi