Matayarisho kwa mashindano ya msururu wa dunia ya mbio za Nyika yaanza Eldoret

Chama cha riadha Kenya kimeanza maandalizi kwa mashindano ya msururu wa dunia ya mbio za Nyika Februari mwaka ujao mjini Eldoret Februari 12 mwaka ujao.

Kulingana na afisa wa kamati kuu ya riadha Kenya , Barnaba Korir tayari, , wamebaini eneo ambapo mbio hizo za kukata mbuga zitakapoandiliwa huku maafisa kutoka shirikisho la riadha ulimwenguni wakitarajiwa kuzuru nchini kukagua mkondo huo.

Also Read
Mwanabiashara maarufu wa Eldoret Jackson Kibor amefariki

“Tayari tumeanzabaini eneo mbio hizo zitaandaliwa nje tu ya mji wa Eldoret na tunasubiri makarani wa mkondo kuanza kupima ,hatua ambayo itafuatiwa na ziara ya maafisa kutoka shirikisho la riadha ulimwenguni ambao watazuru kuidhinisha mkondo.

Tunataka mkondo huo uwe mgumu sawia na ule mashindano ya dunia mwaka 2020 mjini Aarhus Denmark ambao ulikuwa na changamoto nyingi.

Also Read
Viongozi wa kidini wataka kafyu iondolewe usiku wa kuamkia mwaka mpya

Itakuwa ni fursa nzuri kwa wanariadha wa humu nchini na wale wa kimataifa kujipima hususan baada ya mashindano ya dunia ya mbio za nyika mwaka ujao nchini Australia kuahirishwa hadi mwaka 2023″akasema Korir

Itakuwa mara ya kwanza kwa Kenya kuandaa mashindano makubwa ya mbio za nyika tangu mwaka 2007 ilipokuwa mwenyeji wa mashindano ya dunia mjini Mombasa.

Also Read
Washiriki wa Kenya wa Marathon katika michezo ya Olimpiki wapigwa jeki na NOCK

Mashindano hayo ya mikondo 17 ya nembo ya dhahabu yataanza kwa mikondo ya mabara ya Oceania, North America, Ulaya na Asia .

Ni mashindano mapya ya nembo ya dhahabu kuandaliwa nchini baada ya yale ya Kip Keino Classic continental tour.

  

Latest posts

Boro wamtimua meneja Chris Wilder kwa matokeo duni

Dismas Otuke

Malkia Strikers warejea nyumbani kinyemela baada ya kubanduliwa mashindano ya dunia

Dismas Otuke

CAF yafungua maombi ya maandalizi ya fainali za AFCON mwaka 2025

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi