Matayarisho ya Safari Rally yaingia hatua ya lala salama

Matayarisho  kwa  mashindano  ya Safari rally yameingia mkondo wa  lala  salama  mjini Naivasha siku  1 kabla ya kuanza kwa patashika  hiya.

Magari kadhaa  yanaendelea kufanyiwa  ukarabati  na marekebisho  huku pia ujenzi wa  jukwaa  kuu ukikaribia  kukamilika.

Also Read
Watu wanne wafariki katika ajali ya barabarani Bungoma
eneo la mahojiano kwa madereva

 

Mashindano  hayo  yanarejea  kwenye kalenda  ya WRC kwa mara  ya  kwanza  baada ya miaka  19.

Kwa mjibu wa  mmoja wa washirikishi ambaye  pia ni  dereva mwelekezi  mstaafu  Abdul  Sidi wanasubiri  mashindano hayo  kwa  hamu hamamu.

Also Read
Obiri awika katika mita 10000 Kasarani
Abdul Sidi mwelekezi mstaafu  ambaye kwa sasa ni mmoja wa washirikishi

 

“Ni fahari kuu  kuona  mashindano  hayo  yamerejea na kwa kawaida  kutokana  na experience  yangu  yatatoa  nafasi kwa  madereva  wa Kenya kushindana na madereva  bora  ulimwenguni”akasema Sidi

Hali  ya  usalama  imeimarishwa  huku idadi  kubwa ya polisi  ikishika  doria.

Also Read
Buriani Beatrice Kevogo
jukwaa la vip

Mashindano  hayo ambayo  pia yatakuwa ya mkondo wa 6 wa WRC  yataandaliwa baina  ya Juni  24 na 27  na  kurushwa  mbashara  na  runinga  ya  KBC Channel one.

  

Latest posts

Police Fc washerehekea kurejea ligi kuu baada ya mwongo mmoja kwa dhifa

Dismas Otuke

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Vidosho wa Kenya wapigwa dafrao na Msumbiji mashindano ya kikapu Afrika

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi