Matayarisho ya SOYA awards yakamilika

Matayarisho kwa tuzo za mwaka huu za wanamichezo bora nchini SOYA awards yamekamilika katika uwanja wa Bukhungu kaunti Kakamega tarehe 25 mwezi huu.

Kulingana na mwenyekiti wa jopo la uteuzi wa washindi Chris Mbaisi ,tayari wamekamilisha uteuzi wa wanaspoti bora watano katika kila kitengo huku wakitarajia kuwachuja hafi wa tatu wa mwisho.

“Tumefanya Shortlist ya wanaspoti watano bora katika kila kitengo na tunatarajia kupunguza hadi watatu wa mwisho kabla ya siku ya sherehe”

Also Read
Simba wa Nairobi wazidisha machungu ya Mathare United baad ya kuilaza 2-0

“Tulipanga kuandaa hafla hii tarehe 19 mwezi huu lakini tumeisongeza mbele hadi tarehe 25 ili kutoa fursa kwa wanariadha kushiriki mashindano ya kitaifa ya mbio za nyika tarehe 22 Januari mjini Eldoret”
akasema Mbaisi

Kwa mara ya pili mtawalia hakutakuwa na kitengo cha washindi kutoka mashindano ya shule za sekondari baada ya mashindano yote kusitishwa mwaka 2020 kutokana na Covid 19.

Also Read
Wanariadha chipukizi 43 wateuliwa kushiriki mashindano ya dunia mwezi ujao

Vitengo vitakavyowaniwa ni:-mwanamichezo bora wa mwaka kwa jumla,mwanaspoti bora wa mwaka kwa wanaume na wanawake,mwanaspoti bora wa mwaka kwa walemavu wanaume na wanawake,mchezaji chipukizi bora wa mwaka kwa wavulana wasichana na timu bora ya mwaka.


Pia kulingana na Mbaisi ilivyo desturi watamwalika mwanamichezo tajika kuwa mgeni wa heshima.

“Kawaida ya SOYA tutamwalika mchezaji maarufu ,raundi hii akiwa wa kutoka Afrika mashariki kuwa mgeni wa heshima”akasisitiza Mbaisi

Also Read
AK kuandaa majaribio ya kitaifa ya mbio za Relays tarehe 8 mwezi huu

Tuzo za Soya zilianzishwa miaka 18 iliyopita na bingwa mara tano wa dunia katika mbio za nyika Dkt Paul Tergat kwa lengo la kuwatambua na kuwatuza wachezaji wanaonawiri kila mwaka.

Itakuwa mara ya tatu mtawalia kwa hafla hiyo Kuandaliwa katika kaunti,baada ya kuandaliwa katika kaunti za Mombasa na Nakuru katika makala mawili yaliyopita mtawalia.

  

Latest posts

Riadha Kenya kuandaa seminaa kwa wanariadha Januari 21 kutangulia mashindano ya kitaifa

Dismas Otuke

Polisi wachunguza mauaji ya mwanamke aliyepatikana ndani ya sanduku

Tom Mathinji

Kenya haitatuma timu kwa michezo ya Olimpiki ya majira ya Baridi Beijing

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi