Matiang’i asifia mpango wa kazi mtaani

Waziri wa usalama wa taifa Dkt. Fred Matiang’i  ameupongeza mpango wa Kazi mtaani akisema ni bora zaidi katika kuhakikisha ukosefu wa ajira kwa vijana unakabiliwa.

Akizungumza katika eneo la Kasarani wakati alipofungua rasmi afisi za kaunti ndogo ya Kasarani,  Matiangi, ametoa wito kwa vijana ambao wangali hawajanufaika na mpango huo kuwa wavumilivu akisema kuna mpango wa kuhusisha kila moja.

Also Read
Wanafunzi wawili wafariki katika hali tatanishi Nakuru
Also Read
Mgombea wa ODM Pavel Oimeke ashinda uchaguzi mdogo wa Bonchari

Akiwahutubia vijana kuhusiana na mpango huo wa usafi  unaofahamika kama Kazi Mtaani katika eneo la  Kasarani, Matiang’i alisema mpango huo utaimarishwa kuanzia mwaka ujao.

Also Read
Muda wa mpango wa kazi mtaani waongezwa hadi mwezi Machi

Waziri huyo wa usalama wakati huo huo alitoa onyo kali kwa wanyakuzi wa ardhi.

Matiangi alisema serikali itaimarisha doria  kuhakikisha kuna usalama wakati huu na baada ya sherehe za krismasi.

  

Latest posts

Visa 394 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Chris Obure ana kesi ya kujibu kuhusiana na sakata ya Anglo Leasing

Tom Mathinji

Rais Kenyatta atoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa Kilimo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi