Matiang’i: Serikali itashughulikia maswala yanayoathiri ukuzaji na uuzaji Miraa

Serikali imebuni kamati ambayo itahusika na kupigia debe uuzaji wa Miraa katika masoko ya humu nchini na yale ya kimataifa.

Waziri wa usalama wa taifa Dkt. Fred Matiang’i, alisema kamati hiyo inayojumuisha wizara kadhaa na serikali ya kaunti ya Meru, pia itajizatiti kusuluhisha maswala tata yanayoathiri mmea huo.

Waziri huyo alikuwa akizungumza katika kongamano la kisayansi kuhusu Miraa, lililoandaliwa kwa pamoja na serikali ya kaunti ya Meru na taasisi ya kitaifa kuhusu utafiti wa kimatibabu (KEMRI), katika chuo kikuu cha Nairobi.
Matiang’i aliahidi kushirikisha halmashauri ya kitaifa ya kukabiliana na utumizi wa mihadarati (NACADA), kubadilisha uorodheshaji wa miraa ambayo hukuzwa kwa wingi katika kaunti za Embu na Meru kama ‘mihadarati sugu’, akisema uorodheshaji huo haukuungwa mkono na ushahidi wa kisayansi.

Also Read
Visa 108 zaidi vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Wanabiashara wa Miraa, wamelalamikia hatua ya NACADA ya kufanya msako dhidi ya zao hilo na dhuluma za maafisa wa serikali ya kaunti wanaotekeleza sheria inayohusu uorodheshaji wake.

Also Read
Wizara ya afya yatahadharisha kuzuka kwa ugonjwa wa ukambi hapa nchini

Waziri Matiang’i alisema “Katika muda wa miaka miwili au mitatu, tunapaswa kukamilisha swala la uorodheshaji wa miraa. Tunapaswa sasa kuangazia kuwasaidia wakulima wa miraa na wafanyibiashara kupata soko zaidi,”.

kwa upande wake, waziri wa biashara Betty Maina, alisema serikali kwa sasa inaangazia masoko mengine kwa zao hilo huku mashauri yakiendelea na nchi kama Jamuhuri ya Kimekrasia ya Congo DRC, Djibouti, Mozambique, Yemen, na Israel miongoni mwa nchi zingine.

Also Read
Huenda serikali ikawaharamisha wapiganaji wa jamii ya Pokot

Hata hivyo waziri wa kilimo Peter Munya, aliwahimiza wakulima na wanabiashara, kuzingatia uongezaji dhamani na uvumbuzi kwa mmea huo wa miraa.

Gavana wa Meru Kiraitu Murungi, alisema kongamano hilo la siku mbili litakusanya utafiti kuhusu athari za miraa kuhusu Afya, uchumi na kijamii na pia kusaidia kutatua changamoto ambazo zimeghubika sekta hiyo kwa muda mrefu.

  

Latest posts

Kalonzo: baadhi ya walioteuliwa kuwa Mawaziri si waadilifu

Tom Mathinji

George Kinoti amkabidhi mamlaka kaimu mkurugenzi wa DCI Hamisi Massa

Tom Mathinji

Rais Ruto abuni kamati ya kutathmini mtaala wa CBC

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi