Mauaji ya mwanaume mmoja yazidisha taharuki Ol Moran

Taharuki imetanda katika sehemu ya Wangwaci iliyo katika wadi ya Ol Moran,kaunti ya Laikipia baada ya mwanaume mmoja wa umri wa miaka 64 kuuawa siku ya Jumatano kwa kupigwa risasi na watu wanaoshukiwa kuwa majambazi waliojihami.

Washambulizi hao wanaoaminika kutoka eneo linalokumbwa na ghasia la hifadhi ya wanyama pori ya Laikipia, walimuua kwa kumpiga risasi Charles Maina katika sehemu ya Corner Mawe iliyo umbali wa takriban mita mia tano kutoka mahali ambapo kundi la maafisa wa usalama kutoka taasisi mbali mbali linachimba mtaro kando ya barabara ya hifadhi hiyo kutoka Wangwachi hadi Kamwenje.

Also Read
Baba aliyembaka bintiye wa miaka 6 Kisii kufikishwa mahakamani

Majambazi hao baadaye waliiba ngombe 30 na kuelekea katika hifadhi hiyo. Samuel Ruchuiri,ambaye alinusurika shambulizi hilo alisema walikuwa wakiwalisha mifugo wao katika sehemu ya Corner Mawe wakati majambazi waliojihami walipowavizia na kuwashambulia mwendo wa saa tisa alasiri.

Also Read
Serikali yatakiwa kuimarisha usalama katika mpaka wa kaunti za Laikipia na Isiolo

Mwakilishi wadi ya Ol Moran George Karuiru, alishangaa ni vipi serikali inasema imeimarisha hali ya usalama katika hifadhi hiyo, na huku Majambazi  wanajitokeza katika maficho yao na kuwapitisha mifugo walioibwa katika hifadhi hiyo hiyo.

Also Read
Rais Kenyatta awateua watu watano kujiunga na TSC

Kifo hicho kimeongeza hadi 13 idadi ya watu ambao wameuawa katika wadi ya Ol Moran katika muda wa mwezi mmoja uliopita.

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Sipili Funeral home.Oparesheni ya kiusalama inaendelea katika hifadhi hiyo.

  

Latest posts

Idara ya Mahakama yashutumiwa kwa kuhujumu shughuli muhimu za serikali

Tom Mathinji

Uhuru Kenyatta: Usalama wa taifa hili ni shwari

Tom Mathinji

Hospitali ya Kijeshi yazinduliwa katika kambi ya kijeshi ya Kahawa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi