Mazishi ya Othuol Othuol

Mwili wa mchekeshaji Othuol Othuol ambaye jina halisi ni Ben Maurice Onyango utazikwa hii leo nyumbani kwao katika kijiji cha Got Gaga, eneo la Ndere ndani ya Alego kaunti ya Siaya.

Jana asubuhi mapema mwili huo ulitolewa kwenye hifadhi ya maiti ya Chiromo na kuelekezwa kwenye ukumbi wa maonyesho yaani “Kenya National Theatre” ambapo maombi yalifanyika na safari ya kuelekea kaunti ya Siaya ikaanza kama saa nne asubuhi.

Also Read
Fursa ya kicheko kwa wanaotumia lugha ya Ekegusii

Othuol aliaga dunia akiendelea kupata matibabu katika hospitali kuu ya Kenyatta jijini Nairobi jumapili tarehe 11 mwezi huu wa oktoba mwaka 2020 saa kumi na moja unusu jioni.

Also Read
Mchekeshaji Afariki Kwenye Sherehe Marekani

Mwenyekiti wa chama cha wachekeshaji nchini Ken Waudo anasema mazishi ya leo yanaandaliwa kwa kuzingatia kanuni zote za wizara ya afya za kuzuia maambukizi ya Corona.

Jumatano iliyopita usiku, wasanii wenza wakiongozwa na Churchill na Jalang’o walikesha nje ya ukumbi wa maonyesho na kuwasha mishumaa kama njia ya kumkumbuka Othuol Othuol mkutano huo pia ulikuwa wa kuchanga fedha za kufadhili mazishi.

Also Read
Shishi Baby Vs Vanessa Mdee

Wasanii hao wamekanusha tetesi kwamba walitelekeza mwenzao na kuelezea kwamba wamekuwa naye wakati wote akiugua.

  

Latest posts

Rayvanny Kumtambulisha Msanii wa Kwanza NLM

Marion Bosire

Dulla Makabila Ajiondolea Lawama

Marion Bosire

Mwigizaji Atoa Ilani Kwa Rais Museveni

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi