Mbappe asema angali na ndoto ya kucheza Real Madrid siku moja

Licha ya kusaini mkataba mpya wa kusalia na na mabingwa wa Ufaransa PSG,mshambuliz Kylian Mbappe amesema ndoto yake ya kuwachezea mabingwa wa Uhispania Real Madrid ingalipo.

Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 23 alikuwa amehusishwa kuhamia Madrid msimu huu wa uhamisho ,lakini amehiari kusalia Ufaransa baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu.

Also Read
Droo ya makundi ya ligi ya mabingwa Ulaya kuandaliwa Oktoba mosi

Mbappe,ambaye ni mmoja wa wanandinga bora ulimwenguni kwa sasa amesema walizungumza na Rais wa Real Madrid Florentino Perez moja kwa moja na kumfahamisha kuhusu uamuzi wake wa kusaini mkataba mpya na PSG.

Also Read
uchaguzi wa matawi ya Fkf waendelea mbele ilivyopangwa

Mbappe alipachika mabao 28 katika msimu wa ligi kuu Ufaransa ,league 1 uliokamilika wikendi iliyopita.
28 goals in Ligue 1 to help PSG win the title.

Mbappe alianza amali yake ya kupiga soka na klabu ya Monaco ,kabla ya kuhamia PSG mwaka 2017, akianza kwa mkopo kabla ya kupata uhamisho wa kudumu.

Also Read
Kipchoge ahudhuria mechi ya Psg dhidi ya Lille ugani Parc De Princesss

Akiwa PSG Mbappe ameshinda mataji manne ya league 1 na matatu ya kombe la Ufaransa.

  

Latest posts

Mchezaji Sopu Ajiunga na Azam FC

Marion Bosire

Makundi ya wakiritimba yalaumiwa kwa kuficha Mahindi

Tom Mathinji

Visa 108 zaidi vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi