Makala ya tatu ya mbio za Eldoret City Marathon yataandaliwa tarehe 6 mwezi Juni baada ya kuahirishwa kutoka April 11 mwaka huu kufuatia kusitishwa kwa shughuli za michezo nchini na Rais Uhuru Kenyatta.
Akizungumza Alhamisi Gavana wa kaunti ya Uasin Gushu Jackson Mandago ambaye ni mfadhili wa mbio hizo amewataka wanariadha kuendelea kujisajili.
Ni mara kwanza kwa mbio hizo kuandaliwa kwa kutumia mtambo wa kielektroniki wa kupima muda.
Kulingana na mkurugenzi wa mbio hizo Moses Tanui,washiriki zaidi ya 400 wamejisajili wakiwemo 11 wa kimataifa wakiwemo kutoka
Russia, Uganda, Uingereza , Argentina na Ethiopia.
Mshindi wa mbio hizo atatuzwa shilingi milioni 3 nukta 5 huku wanariadha wa kwanza 20 kwa wanaume na wanawake wakituzwa.
Valary Aiyabei alishinda makala ya mwaka 2019 aliposajili muda wa saa 2 dakika 27 na sekunde 17 huku Mathew Kisorio akitwaa ubingwa kwa wanaume kwa saa 2 dakika 12 na sekunde 38 .