Mbosso atoa albamu

Mwanamuziki wa Tanzania Mbwana Yusuph Kilungi ambaye wengi wanamfahamu kama Mbosso ametoa albamu yake ambayo ilikuwa ikitarajiwa na wengi iitwayo “Definition of love”.

Mapema asubuhi hii leo, Mbosso alitoa orodha ya nyimbo ambazo ziko kwenye albamu hiyo ambayo ndiyo yake ya kwanza. Nyimbo hizo ni 12 na zinajulikana kama; Mtaalam, Kiss Me, Baikoko ambao amemhusisha Diamond Platnumz na Tulizana ambao aliimba na Njenje wa bendi ya Kilimanjaro.

Also Read
Rayvanny kuzindua albamu

Wimbo wa tano kwenye albamu hiyo unaitwa Yalah, wa sita Sakata ambao aliimba na Flavour, wa saba Pakua aliouimba na Rayvanny ambaye pia ni wa kundi la WCB na wa nane ni Karibu ambao aliimba tena na Diamond.

Nyimbo nyingine ni Your Love ambao aliimba na Liya, Kadada alouimba na Darassa, Yes wake na Spice Diana na Nipo Nae ambao ameimba peke yake.

Also Read
Rick Ross Azungumzia Uhusiano Wake na Hamisa Mobeto

Aliongezea nyimbo nyingine mbili ambazo anarejelea kama “Bonus Tracks” mmoja unaitwa Limevuja na mwingine Kamseleleko ambao alimshirikisha Baba Levo.

Mbosso ambaye sasa ana umri wa miaka 30 alianza kuimba kwenye kundi ambalo lilifahamika kama “Yamoto Band” na liliposambaratika akarejea kijijini ambako alikosa namna ya kuendelea hadi mwaka 2014 alipoitwa na Diamond Platnumz ili amsaidie kurejelea muziki.

Akiwa chini ya WCB, Mbosso alitoa wimbo wake wa kwanza uitwao “Watakubali” tarehe 28 mwezi januari mwaka 2018 na kesho yake akatambulishwa rasmi kama mwana WCB.

  

Latest posts

Shona Ferguson Ashinda Tuzo Hata Baada Ya Kifo

Marion Bosire

Snoop Dogg Atangaza Kifo Cha Mamake

Marion Bosire

Etana Kutumbuiza Nairobi

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi