Mbunge Sir David Amess auawa kwa kudungwa kisu nchini Uingereza

Mbunge mmoja wa chama cha Conservative nchini Uingereza, Sir David Amess amefariki baada ya kudungwa kisu wakati wa kikao cha kukutana na watu wa eneo bunge lake huko Essex.

Duru za Polisi zimearifu kwamba mtu mmoja mwenye umri wa miaka 25 alikamatwa baada ya kushukiwa kwa mauaji kufuatia tukio hilo kwenye kanisa moja katika eneo la Leigh-on-Sea.

Also Read
Israeli yaonya kuhusu ufaafu wa Rais Mteule wa Iran Ebrahim Raisi

Walisema walipata kisu kimoja na kwamba hawamtafuti mtu mwingine yeyote kuhusiana na kisa hicho. Sir David, aliyekuwa akiwakilisha eneo la Southend West, alikuwa akiongoza kikao cha kusikiza malalamishi ya wakaazi wa eneo-bunge lake –kwenye kanisa la Ki-Methodisti la Belfairs lililoko katika eneo la Eastwood Road North.

Also Read
Joe Biden: Nitaliunganisha taifa la Marekani

Sir David, mwenye umri wa miaka 69, amekuwa mbunge tangu mwaka 1983 na pia ana mke na watoto watano.

Yeye ni mbunge wa pili aliye mamlakani kuuawa katika muda wa miaka mitano, baada ya mauaji ya Mbunge mwingine wa chama Labour Jo Cox mnamo mwaka 2016.

Also Read
Washukiwa wanne wa mauaji ya Rais wa Haiti Jovenel Moïse wauawa na polisi

Mbunge huyo aliuawa nje ya maktaba moja huko Birstall, West Yorkshire, ambako alikuwa amepangiwa kuongoza kikao cha kusikiliza malalamishi ya wakaazi wa eneo-bunge lake.

  

Latest posts

Serikali ya mpito ya Sudan yahimiza kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa

Tom Mathinji

FOCAC yanyanyua wakulima wa Afrika kimapato na kuondokana na umasikini

Tom Mathinji

Riek Machar ashinikiza kubuniwa jeshi la pamoja kabla ya Uchaguzi Mkuu Sudan Kusini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi