Mbunge wa Kigumo Wangari Mwaniki asema BBI itaimarisha uchumi wa nchi

Mbunge wa Kigumo Wangari Mwaniki ameusifu mpango wa maridhiano ya kitaifa, BBI, akisema kuwa ripoti hiyo, iwapo itapitishwa, itaimarisha ukuaji wa kiuchumi humu nchini.

Akiongea kwenye Eneo-Bunge lake, Mwaniki amesema kuwa mchakato wa BBI, mbali na kutaka kuleta ujumuishaji na umoja wa kitaifa, utaleta amani nchini.

Amesema kuwa utulivu humu nchini utasaidia kuwavutia wawekezaji na kuimarisha ukuaji wa kiuchumi.

Mbunge huyo amehoji kuwa katika nyakati za awali, baadhi ya kampuni ziliamua kuhamisha biashara zao kutoka humu nchini kwa kuhofia ghasia ambazo huzuka mara kwa mara baada ya uchaguzi kuandaliwa.

Also Read
EACC yakamilisha awamu ya kwanza ya uchunguzi dhidi ya KEMSA

Mwaniki ametoa wito kwa wanasiasa wasitumie vibaya ripoti hiyo ya BBI kusababisha migawanyiko miongoni mwa Wakenya, akisema kuwa wale walio na maoni tofauti wanafaa kusikizwa na marekebisho yafaayo kufanywa kabla ya kupitishwa kwa ripoti hiyo.

“Tunafaa kusikizana na tuwe na mjadala mzuri kuhusu BBI. Ripoti hiyo kulingana na mimi ni nzuri kwa nchi hii na kila mmoja anafaa kuhusika,” akasema mbunge huyo.

Also Read
Mgodi wa Macalder waua tena

Mbunge huyo ameongeza kuwa nchi hii itaafikia viwango vya juu vya maendeleo iwapo uongozi na siasa zitawekewa misingi katika amali.

Amepinga kauli ya wengine kwamba ripoti hiyo ina nia ya kutengenezea wanasiasa Fulani nafasi serikalini, akisema kuwa nafasi za Waziri Mkuu na manaibu wawili zitahakikisha kwamba jamii zaidi zinahusika katika serikali.

Aidha, Mwaniki amesema kipengee cha kuongezwa kwa mgao wa fedha za kaunti kutoka asilimia 15 hadi 35 kutahakikisha maendeleo zaidi magatuzini, hasa kupitia kubuniwa kwa hazina ya maendeleo ya wadi.

Also Read
Serikali kuharamisha utumizi wa kahawa kama dhamana ya mikopo

Amewataka Wakenya wajisomee ripoti hiyo na kuielewa, badala ya kukubali kupotoshwa na wanasiasa.

“Wananchi wasome na waelewe ripoti hii kabla kufanya maamuzi. Nawasihi wanasiasa wenzangu tukome kuwapotosha wananchi kuhusu ripoti hiyo. Wakenya wana uwezo wa kusoma na kuelewa ripoti hiyo bila ushawishi mkubwa,” akaongeza.

 

  

Latest posts

Mutahi Kagwe: Wahudumu wa afya wafeli katika somo la Kingereza

Tom Mathinji

Prof Magoha: Awamu ya kwanza ya ujenzi wa madarasa ya CBC kukamilika mwezi Aprili mwakani

Tom Mathinji

Benki ya dunia kuipa Kenya shilingi bilioni 16.7 kukabilia na ukame

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi