Mchimba mgodi afariki katika kaunti ndogo ya Bondo

Mtu mmoja alifariki Alhamisi alasiri kwenye mgodi wa dhahabu wa Kachola, kijijini Buoro, kaunti-ndogo ya Bondo.

Mhasiriwa huyo mwenye umri wa miaka 43 alifariki papo hapo baada ya kugongwa kichwani na mwamba kwenye shimo la mgodi huo dhahabu.

Kulingana na Edwin Ooro ambaye pia alikuwa akifanya kazi na mhasiriwa kwenye shimo hilo la mgodi, kulikuwa na wachimbaji wanne wa migodi katika shimo hilo la kina cha futi 30 wakati wa mkasa huo.

Also Read
Wakenya wahimizwa kupuuza dhana potovu dhidi ya Chanjo za kukabiliana na Covid-19

Ooro alidokeza kwamba marehemu alikuwa kwenye harakati za kutoka nnje ya mgodi alipoghumbana na mauti.

Chifu wa eneo la Bondo Township, Walter Omolo, ambaye alithibitisha kisa hicho  alisema alipashwa habari na naibu wa Chifu wa sehemu hiyo, na alipowasili mahala hapo  alipata mwili wa marehemu ukiwa tayari umeondolewa kwenye shimo la mgodi.

Also Read
Watu 11 zaidi waambukizwa Covid-19 hapa nchini

Chifu Omolo alisema migodi yote katika eneo hilo inaendeshwa kinyume cha sheria baada ya serikali kuharamisha shughuli hizo.

Ajali hiyo inajiri wiki mbili baada ya wachimbaji wanane wa migodi kunaswa kwenye mgodi wa dhahabu wa Abimbo umbali wa kilomita 30 kutoka mahala hapo, katika eneo hilo hilo la Bondoa.

Also Read
Askofu wa Legio Maria afariki katika hali tatanishi kaunti ndogo ya Bondo

Sita kati yao waliokolewa wakiwa hai, ilhali mmoja bado amenaswa kwenye mgodi huo wa kina cha futi 500, mbali na mwili wa mmoja wa wachimbaji migodi hao ambao pia iliondolewa.

Mwili wa yule aliyefariki kwenye ajali ya leo alasiri ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Bondo.

  

Latest posts

Dereva na Makondakta wawili watiwa nguvuni kwa kukiuka sheria za trafiki

Tom Mathinji

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi