Meja Jenerali Francis Ogolla ateuliwa naibu Mkuu wa vikosi vya ulinzi

Rais Uhuru Kenyatta amefanya mabadiliko kwenye vikosi vya ulinzi vya Kenya. Akiwa amiri jeshi mkuu wa vikosi vya ulinzi nchini Rais Kenyatta amempandisha cheo Meja Jenerali Francis O. Ogolla kwa cheo cha luteni Jenerali na kumteua kuwa naibu mkuu wa vikosi vya ulinzi.

Ogolla ambaye amekuwa kamanda wa vikosi vya wanaanga, amechukua mahala pa luteni Jenerali Frankline L. Mghalu ambaye kipindi chake cha kuhudumu kimekamilika baada ya kuhudumu kwa miaka 40.

Also Read
Wauguzi 69 wafurushwa kutoka nyumba za serikali ya Kaunti ya Taita Taveta

Rais pia amempandisha cheo meja Jenerali Mohammed Badi kwa cheo cha luteni Jenerali na atasalia kuwa mkurugenzi mkuu wa halmashauri ya usimamizi wa eneo la jiji la Nairobi.

Kadhalika Brigadier John Omenda amepandishwa chezo cha Meja Jenerali na kuteuliwa kuwa kamanda wa vikosi vya wanaanga.

Also Read
Rais Kenyatta amwomboleza Orie Rogo Manduli

Meja Jenerali Albert Kendagor amepandishwa cheo hadi luteni Jenerali na kuteuliwa kuwa kamanda mteule wa kikosi cha AMISOM huku  Meja Jenerali Jonah Mwangi akipandishwa cheo hadi luteni Jenerali na kuteuliwa kwa chansela wa chuo kikuu cha kitaifa cha mafunzo ya ulinzi nchini .

Meja Jenerali William Shume ameteuliwa kuwa kamanda wa jeshi la Kenya kuchukua mahala pa Meja Jenerali Kendagor.

Also Read
Uhusiano kati ya Kenya na Ethiopia kuimarishwa huku Kituo cha Mpakani cha Moyale kikizinduliwa

Mabadiliko hayo yalitangazwa siku ya Ijumaa kufuatia mapendekezo ya baraza la ulinzi chini ya mwenyekiti Monica Juma ambaye ni Waziri wa ulinzi.

Katika mabadiliko hayo msemaji wa vikozi vya ulinzi sasa ni Kanali Esther Wanjiku anayechukua mahala pa Kanali  Zilporah Kioko aiyekwenda kwa masomo zaidi.

  

Latest posts

Shule za umma zina uwezo wa kuandikisha matokeo bora iwapo zitajikakamua zaidi

Tom Mathinji

Mzozo wa kidiplomasia kati ya Uchina na nchi za magharibi wasitishwa

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi apuuzilia mbali dhana ya ma-‘Hustler’

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi