Mercy Johnson aelezea sababu za kuacha majukumu ya kimapenzi katika uigizaji

Mercy Johnson Okojie amabaye ni mmoja wa waigizaji tajika wa filamu za Nigeria ameelezea sababu za kuacha kuigiza sehemu ambazo zina vitendo vya mapenzi.

Wanaopenda kutizama filamu za Nollywood wanajua kwamba Mercy huigiza katika kila jukumu analopatiwa isipokuwa la kimapenzi hasa kabla na baada ya kuolewa yapata miaka tisa iliyopita.

Ameigiza kama msaidizi wa nyumbani, msaidizi katika makazi ya mfalme, mke au mpenzi aliyetelekezwa, mtoto wa kambo anayeteswa, mnyanyasaji kijijini kati ya sehemu nyingine nyingi.

Wafuasi wake katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakitaka kujua ni kwa nini haigizi sehemu zilizo na vitendo vya mapenzi na akaamua kuwapa jibu.

Mercy alisema ni kwa sababu ya mume wake Prince Odianosen Okojie. Kulingana naye mume wake hapendelei kumwona akiigiza sehemu za kimapenzi. Jambo lingine alilolisema Mercy ni kwamba angetaka watoto wake na watoto wengine katika jamii wajifunze toka kwake.

Mercy na mume wake

 

Also Read
Tina Knowles-Lawson amkashifu Piers Morgan
Also Read
Muigizaji wa Nollywood Bruno Iwuoha ameaga dunia

Mercy alianza kuigiza mwaka 2004 punde tu baada ya kumaliza masomo ya shule ya sekondari. Tangu wakati huo amekua katika nyanja ya uigizaji na sasa ni muigizaji tajika. Aliwahi kushinda tuzo la muigizaji msaidizi bora mwaka 2009.

Aliolewa mwaka 2011 na Prince Odianosen Okojie na pamoja wamejaliwa watoto wanne.

 

Also Read
Crazy Kennar azindua mkahawa
Familia ya Mercy

Mercy anajulikana sana kwa pupenda kufanya mazoezi jambo ambalo limeufanya mwili wake kuwa wa kuvutia.

  

Latest posts

Yul Edochie Amsifu Babake

Marion Bosire

Aki Na Paw Paw Warejea

Marion Bosire

Harmonize Atoa Orodha Ya Nyimbo Za Albamu Mpya

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi