Meya wa jiji la London nchini Uingereza ameelezea wasi wasi wake kuhusu hali ya Covid-19 mjini humo, hii ikiwa ni baada ya kunakili ongezeko la visa vya ugonjwa huo siku ya Ijumaa.
Sadiq Khan alisema visa hivyo vipya 26,000, vinaonekana kuwa na athari kubwa kutokana na ukosefu wa wahudumu wa dharura mjini humo.
Takwimu za hivi punde za serikali zinaonyesha kuwa idadi ya wagonjwa waliolazwa hospitalini jijini London ni 1,534, hili likiwa ni ongezeko la asilimia 28.6 katika muda ya juma moja lililopita.
Mawaziri wameambiwa kwamba huenda sheria mpya za kuthibiti chamko hilo zikahitajika ili kuiepusha Uingereza kutolaza hospitalini zaidi ya wagonjwa 3,000 kwa siku.
Shirika la afya elimwenguni nimesema kuwa aina mpya ya virusi vya COVID-19, Omicron,imethibitishwa katika takriban nchi 89 na inasambaa kwa kasi sana kuliko ile ya Delta.
Shirika hilo limeongeza kuwa inaenea kwa kasi sana katika mataifa yaliyo na idadi kubwa ya watu.