Mfanyibiashara mashuhuri wa china Sun Dawu afungwa miaka 18 gerezani

Bwanyenye  mmoja mashuhuri  nchini  China amehukumiwa kifungo cha miaka 18 gerezani, ikiwa ni adhabu ya hivi karibuni dhidi ya wakubwa wa makampuni wanaokosoa serikali.

Sun Dawu anaendesha moja ya biashara kubwa zaidi ya kilimo nchini humo  katika mkoa wa kaskazini wa Hebei.

Sun, mwenye umri wa miaka 67,  awali  amewahi kutoa maoni  kuhusu swala la haki za binadamu ambalo ni  mada nyeti kisiasa. Alipatikana na hatia ya “kuzua ugomvi na kuchochea ghasia”, shtaka linalotumiwa mara nyingi dhidi ya wanaharakati wanaokosoa serikali nchini humo.

Mashtaka mengine ni pamoja na kujipatia shamba kinyume cha sheria, kukusanya umati wa watu kwa lengo la kushambulia asasi za serikali na kuwazuia wafanyikazi wa serikali kutekeleza majukumu yao.

Pia alitozwa faini ya Dola za Marekani   478,697. Kampuni ya Sun ni miongoni mwa kampuni kubwa zaidi nchini China, na ina  biashara kama vile  utayarishaji wa  nyama na  vyakula vya  wanyama hadi pia  shule na hospitali.

Inasemekana Sun ana uhusiano wa  karibu na wapinzani mashuhuri wa kisiasa wa serikali ya  China na hapo awali  alikosoa sera za serikali  hiyo kuhusu maeneo ya mashambani.

Alikuwa mmoja wa watu wachache walioshutumu wazi serikali kwa kuzuia utoaji wa habari kuhusiana na chamko la homa ya Nguruwe, ambayo iliathiri mashamba yake mnamo 2019, na baadaye ikaharibu  sekta   kubwa ya viwanda  nchini humo.

  

Latest posts

Mauaji ya mwanaume mmoja yazidisha taharuki Ol Moran

Tom Mathinji

Mgomo wa wahudumu wa afya wasababisha maafa Guinea Bissau

Tom Mathinji

IEBC kuongeza Idadi ya nchi za ugenini ambako wakenya watashiriki kwa upigaji kura

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi