Mfumo wa kuhifadhi mazao katika mabohari wazinduliwa nchini

Mfumo wa wakulima kuwasilisha mazao ya kilimo kiuhifadhiwa katika mabohari nchini umezinduliwa rasmi humu nchini ili kuwawezesha wakulima kuweka mazao yao na kupewa risiti za kudhibitisha hatua hiyo.

Stakabadhi zinazotolewa kwa wakulima wanaowasilisha mazaio yao zinaweza kuuzwa au kutumika kutafuta pesa na pembejeo za kilimo.

Also Read
Serikali yaimarisha uvuvi kwenye vina virefu baharini

Waziri wa kilimo  Peter Munya alisema kuwa mfumo huo utasaidia kupunguza hasara za baada ya mavuno kutoka kiwango cha sasa cha asilimia  40 hadi asilimia kumi na kuimarisha mapato ya wakulima.

Halmashauri ya chakula na kilimo nc hini imeidhinisha na kusajili maghala 45 chini ya mfumo huo.

Also Read
Watu 10 zaidi wafariki kutokana na Covid-19 hapa nchini

Maghala ya Halmashauri ya kitaifa ya nafaka na mazao katika maeneo ya   Kitale, Eldoret, Meru, Nakuru na  Nairobi yameanza kupokea mazao ya wakulima.

Mipango inafanywa kujumuisha viazi na kahawa katika mfumo huo mpya ambao sasa unashughulikia nafaka pekee, na ambao unalenga kukabiliana na madalali wanaowapunja wakulima.

Also Read
Serikali yapunguza bei ya pembejeo za Kahawa

Halmashauri ya uwekezaji nchini inatarajia kuanzisha mwongozo wa uwekezaji  kwa watu wanaotaka kuwekezakatika nyanja hiyo kuhusu nafasi zilizoko katika upande wa mabohari.

  

Latest posts

Kamati ya Kusaidia Rais Mteule Kuchukua Hatamu za Uongozi Yaanza Kazi Rasmi

Marion Bosire

Didmus Barasa Ajisalimisha kwa Maafisa wa Polisi

Marion Bosire

Gavana Mandago Sasa ni Seneta

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi