Mfungwa aliyehukumiwa kuhusiana na shambulizi la Chuo Kikuu cha Garissa ajitia kitanzi

Mfungwa mmoja katika Gereza la Kamiti anayetumikia kifungo cha maisha kuhusiana na shambulizi la kigaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa amejitoa uhai.

Ripoti ya polisi inasema kuwa Rashid Charles Mberesero, ambaye ni raia wa Tanzania, alijiua kwa kutumia kamba ya kujitengenezea kwa kutumia blanketi.

Also Read
Ni mwanafunzi mmoja aliyeambukizwa covid-19 tangu kufunguliwa kwa shule

Ripoti hiyo pia inasema kuwa marehemu alikuwa akihudumiwa kutokana na matatizo ya kiakili.

Mberesero na wengine wawili, Mohamed Ali Abikar na Hassan Edin Hassan, walipatikana na hatia kuhusiana na shambulizi hilo mwezi Juni mwaka uliopita.

Also Read
Visa 444 zaidi vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Jaji Francis Andayi wa Mahakama Kuu aliamua kwamba upande wa mashtaka ulithibitisha kikamilifu kwamba watatu hao walipanga shambulizi hilo.

Mshukiwa wa nne wakati huo, Sahal Diriye Hussein, alindolewa lawama kutokana na ukosefu wa ushahidi.

Also Read
Idadi ndogo ya watu wajisajili kuwa wapiga kura Murang'a

Shambulizi hilo lilitekelezwa tarehe 12 mwezi Aprili mwaka wa 2015 katika Chuo Kikuu cha Garissa na kusababisha vifo vya watu 148 huku wengine 79 wakijeruhiwa.

  

Latest posts

Wafungwa watoroka katika gereza la Nanyuki usiku wa manane

Tom Mathinji

Visa 323 vipya vya COVID-19 vyathibitishwa hapa nchini

Tom Mathinji

Ujenzi wa reli kati ya Mai Mahiu na Longonot wakamilika

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi