Mgeni Njoo mwenyeji apone!

Ndiyo hali ambayo imejitokeza wazi kwenye ziara ya Koffi Olomide nchini Tanzania ambako alikuwa amealikwa na “The African Princess” Nandy.
Koffi alitua nchini Tanzania usiku wa kuamkia Jumanne tarehe 26 mwezi huu wa Januari mwaka 2021 ambapo alilakiwa na Nandy kwenye uwanja wa ndege.

Baadaye Nandy aliweka video kwenye akaunti yake ya Instagram akiwa kwenye meza ya maankuli pamoja na Mopao na watu wengine huku akimpakulia Mopao chamcha.

Also Read
Super Unfair! Babu Tale azomewa na mwanawe.

Mwanamuziki huyo alisifiwa sana kwa kuonyesha hulka za mke nyumbani lakini akajipata pabaya kutokana na vyombo vyake ambavyo wengi walionelea sio vya mtu wa hadhi yake.

Mfuasi wake mmoja kwa jina Cleo.Doctor anamwandikia, “Kumbe na mastaa mnatumia mapoti kama yetu”. Mwingine anayejiita Selu_Jo akamwandikia, “Ma super star jamani hata table mats hakuna????….dah mnaboa sana …table setting ovyo kabisa”.

Lakini hali hiyo imegeuka na kuwa baraka kwake kwani sasa amepatiwa vyombo bure kutoka kwa maduka ya kuuza vyombo nchini Tanzania.

Nandy alipachika video kwenye akaunti yake ya Instagram ikionyesha mpangilio wa baadhi ya vyombo hivyo vipya vya kuvutia, vingine vikiwa vya dhahabu.

Kwenye mojawapo ya video akipokea vyombo hivyo, Nandy anasikika akigusia jinsi amechambwa kwenye mitandao mpaka sasa imebidi awe makini sana. Anasikika akisema anatamani kukimbia chumbani aone kama kitanda kiko sawa kabla kionekane na wote.

Koffi alikwenda Tanzania kwa ajili ya kufanya video ya wimbo wake na Nandy.

  

Latest posts

KFCB Yazuia Usambazaji Wa Filamu

Marion Bosire

Eduswagga Azungumzia Safari Yake Ya Muziki

Marion Bosire

Tory Lanez Afuta Instagram Kulikoni?

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi