Mahakama ya kushugulikia kesi za mizozo ya kikazi imeahirisha mgomo unaoendelea wa wafanyikazi wa hospitali kuu ya Kenyatta.
Mahakama hiyo imesitisha mgomo huo hadi kusikizwa na kuamuliwa kwa kesi iliyowasililishwa na hospitali hiyo.
Kesi hiyo itasikizwa tarehe 6 mwezi ujao.
Wafanyikazi wa hospitali hiyo waligoma kwa madai kwamba hospitali hiyo haijatekeleza maafikiano ya kuongeza mishahara yao.
Mahakama iliagiza wasimamizi wa hospitali hiyo kuwafahamisha wafanyikazi hao uamuzi huo kufikia Jumatano jioni.
Hayo yanajiri huku shughuli katika hospitali hiyo zikilemezwa kwa siku ya pili baada ya zaidi ya wafanyikazi wake 5,000 kugoma.
Wafanyikazi hao wanataka utekelezaji wa maafikiano ya nyongeza ya mishahara yao yalioafikiwa mwaka 2012.