Mgomo wa wahudumu wa afya wasababisha maafa Guinea Bissau

Zaidi ya watu 30 wamefariki kutokana na mgomo wa wahudumu wa afya nchini Guinea-Bissau.

Mgomo huo umelemaza kabisa shughuli katika hospitali mbalimbali nchini humo kwa mujibu wa msemaji wa chama cha wauguzi nchini humo.

Mgomo huo wa kususia kazi kutokana na mazingira duni ya kazi, na kushinikiza nyongeza ya mishahara miongoni mwa maswala mengine ulianza siku ya jumatatu katika taifa hilo la Afrika magharibi.

Also Read
NCIC kuwatumia vijana kuwa mabalozi wa amani kabla ya msimu wa uchaguzi

Msemaji wa chama cha wahudumu hao wa afya Garcia Batican Sampaio, aliwaambia wanahabari kuwa anailaumu serikali kwa masaibu hayo.

Also Read
Uhispania yawasamehe viongozi 9 wa Catalonia wanaoshinikiza kujitenga

Msemaji wa serikali Fernando Vaz alisema kuwa wale waliochangia kusababisha vifo hivyo watashtakiwa.

Inadaiwa kuwa taasisi nyingi za matibabu hazina umeme na maji huku kukiwa na kiwango cha juu cha vifo vya kina mama na watoto wakati wa kujifungua.

Also Read
Wakulima wa pamba Lamu waiomba serikali kuwapa ruzuku ya pembejeo ili kuimarisha faida

Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya umoja wa mataifa ya mwaka wa 2017 kuhusu haki za binadamu.

  

Latest posts

Idara ya Mahakama yashutumiwa kwa kuhujumu shughuli muhimu za serikali

Tom Mathinji

Uhuru Kenyatta: Usalama wa taifa hili ni shwari

Tom Mathinji

Hospitali ya Kijeshi yazinduliwa katika kambi ya kijeshi ya Kahawa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi