Miaka mitano gerezani kwa AmberRutty, Said na James au faini ya milioni 11!

‘Amber Rutty’, mpenzi wake Said Bakary na James Charles (James Delicious) wamehukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani au walipe faini ya jumla ya Milioni 11 za Tanzania.

Walipatikana na makosa matatu ikiwemo kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Msanii Rutyfina Abubakary au ukipenda Amberutty na wenzake walishindwa kulipa faini mara moja wakapelekwa gerezani na ikiwa watalipa wataachiliwa.

AmberRutty na mume wake Said

 

“Nimezingatia hoja za pande zote mbili na ATHARI za makosa haya, ni kweli washitakiwa wote vijana na wanategemewa, nimeona mshitakiwa wa kwanza anajutia” Hakimu

Also Read
Nonini na Chipukeezy Wakutana Marekani

‘Mshtakiwa wa Kwanza, Pili na Tatu ni wakosaji wa kwanza, kutokana na mazingira ya kesi hii adhabu yake ni miaka 30 kila kosa ambapo nikiwafunga mtapotea kabisa” Hakimu

“Hivyo kwa mazingira mliyoyasema na lengo la adhabu ni kujirudi, mshitakiwa wa kwanza Utalipa Milioni 3 ama jela miaka 5, mshitakiwa wa Pili utalipa faini ya Milioni 3 ama jela miaka 5 na mshitakiwa wa tatu faini Milioni 5 ama jela miaka 5 adhabu zitaenda sambamba” Hakimu

Also Read
Akothee azua mjadala mitandaoni

Amberutty alijitetea akisema “Naiomba mahakama inipunguzie adhabu nina watoto wananitegemea, mmoja ana matatizo ya Pumu, wazazi wangu pia wananitegemea, alafu naugua T.B inanisumbua,”

Said Bakary naye aliomba mahakama isimpe adhabu kali kwani yeye ni kifungua mimba anayetegemewa kwa familia ya watoto watatu, kwamba mamake amezeeka na anaugua TB anatumia vidonge.

Also Read
Firirinda Weekend!

James kupitia Wakili wake alijitetea akisema ndio mara ya kwanza kupatikana na hatia hivyo basi apewe adhabu ndogo na kwamba ameshirikiana na polisi na mahakama tangu mwanzo wa kesi.

James Delicious

Mwaka 2018 video ya watatu hao wakishiriki tendo la ndoa kinyume na maumbile ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na baadaye Amber na Said wakafunga ndoa ambayo Amber anasema haikudumu.

  

Latest posts

Filamu ya Kenya yashinda tuzo nchini Nigeria

Tom Mathinji

Just A Band yarejea tena baada ya kimya cha muda

Tom Mathinji

Yul Edochie Azungumzia Ndoa Yake ya Wake Wawili

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi