Mifumo hafifu ya sheria yalaumiwa kwa ongezeko la dhuluma za kimapenzi kwa watoto

Wadau wa masuala ya watoto wametoa wito wa kuimarishwa kwa mfumo wa kisheria ili kukabiliana na ongezeko la visa vya ubakaji wa watoto na mimba za mapema humu nchini.

Peter Maina,ambaye ni afisa wa shirika la kukabiliana na majanga barani Afrika ADM, alisema sheria inapasa kutoa adhabu kali kwa washukiwa wa ubakaji.

Aliongeza kusema kwamba vyombo vya habari vinapasa kupeperusha habari sahihi kuhusu visa hivyo kwasababu wanaohusika navyo ni jamaa na marafiki wa waathiriwa.

Also Read
Kongamano kuhusu ugatuzi laahirishwa

Alisema licha ya visa vingi vya mimba miongoni mwa wasichana wa umri mdogo vilivyoripotiwa wakati huu wa janga la COVID 19, ni visa vichache mno vilivyo mahakamani kwasababu ya uandishi duni wa habari.

“Idadi ya mimba miongoni mwa wasichana wadogo ni ya kusikitisha. Maelfu ya wasichana wadogo waliopata watoto wameshindwa kurejea shuleni kutokana na unyanyapaa. Wengi wao walitungwa mimba na jamaa wao au marafiki wakaribu wa familia yao,” alifoka Maina.

Also Read
Wataalam wa WHO wawasili Wuhan kuchunguza chanzo cha Covid-19

Alisema kulingana na utafiti uliofanywa mwezi march mwaka uliopita na mwaka huu,kaunty za Kilifi, Machakos, Nairobi na za magharibi mwa kenya na katikati mwa nchi, zilinakili visa vingi vya mimba miongoni mwa wasichana wa umri mdogo wa kati ya miaka 12 na 16.

Also Read
Marufuku ya usafiri yaliyowekewa kaunti tano yaondolewa

“Ikiwa wanaotekeleza uovu wao wataachiliwa kwa dhamana, basi dhamana hiyo inapaswa kuwa ya mamilioni ya pesa ili kuwazuia wengine kutekeleza uovu huo. Kwa sasa baadhi ya wabakaji wanaachiliwa kwa dhamana ya chini ya shilingi 10,000 huku wengine wakitatulia visa hivyo nje ya mahakama iwapo jamaa au marafiki wanahusika. Hii inapaswa kukomeshwa,” alisema Maina.

  

Latest posts

Mauaji ya mwanaume mmoja yazidisha taharuki Ol Moran

Tom Mathinji

Mgomo wa wahudumu wa afya wasababisha maafa Guinea Bissau

Tom Mathinji

IEBC kuongeza Idadi ya nchi za ugenini ambako wakenya watashiriki kwa upigaji kura

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi