Mikahawa inayokiuka masharti ya kudhibiti Covid-19 kuchukuliwa hatua

Wahudumu wa maeneo ya burudani pamoja na mikahawa wanakabiliwa na hatari ya kupokonywa leseni za kuhudumu kwa muda wa mwaka moja ikiwa, watakaidi masharti ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya Covid-19.

Hayo yalitangazwa na Waziri wa Utalii Najib Balala alipozindua hatua mpya zitakazozingatiwa katika sekta hiyo ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa Covid-19.

Waziri huyo amesema kuzingatiwa kwa sheria hizo kutasaidia kuhakikisha sekta ya utalii inaendelea kuhudumu wakati wa janga hilo.

Also Read
Rais Kenyatta kuongoza taifa kuadhimisha siku kuu ya Jamuhuri

wahudumu wa maeneo ya burudani pamoja na mikahawa wanakabiliwa na hatari ya kupokonywa leseni za kuhudumu kwa muda wa mwaka moja ikiwa watakaidi masharti ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya Covid-19.

Sheria hizo pia zinahitaji sekta hiyo kuhakikisha wageni wanaozuru maeneo hayo wanadhibitishwa kwamba hawajaambukizwa ugonjwa huo wakati wa kuwasili na wakati wa kuondoka bila kujali ikiwa wamepata chanjo dhidi ya COVID-19 au la.

Also Read
COVID-19: Kenya yanakili visa vipya 72 vya maambukizi

Waziri huyo aliongeza kuwa nchi zilizo na Idadi kubwa ya raia waliochanjwa, ndizo zitakazopokea Idadi kubwa ya watalii kwa kuwa nchi hizo zitaashiriwa kuwa zilizo salama kiafya.

Also Read
Watu 469 wapatikana na korona huku kiwango cha maambukizi kikiwa asilimia 11.2

Katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu, Kenya imepokea watalii 300,000 pekee kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta JKIA.

“Wafanyikazi katika sekta ya hoteli na mikahawa wanapaswa kuchukuliwa kuwa walio katika mstari wa mbele kwa kuwa wanawashughulikia wageni wa kiwango cha juu. Ndiposa tunawahimiza wahudumu hao kuchanjwa dhidi ya Covid-19,” alisema Balala.

  

Latest posts

Wanasiasa waonywa dhidi ya kuvuruga amani hapa nchini

Tom Mathinji

Watu wawili wafariki baada ya mashua kuzama Homa Bay

Tom Mathinji

Bunge lachunguza nyongeza ya bei za mafuta

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi