Millicent Omanga Ashukuru Watu wa Nairobi Huku Akikubali Kushindwa

Millicent Nyaboke Omanga amekubali matokeo ya kinyang’anyiro cha uwakilishi wa kaunti ya Nairobi bungeni kulingana na majibu ambayo yalitangazwa leo asubuhi. Kupitia mitandao ya kijamii, mwanasiasa huyo wa chama cha UDA ambacho kiko kwenye muungano wa Kenya Kwanza alishukuru watu wote wa kaunti ya Nairobi, waliompigia kura na ambao hawakumpigia kura.

Also Read
Mahakama ya Kericho yafungwa kwa muda

“Ninakubali matokeo hata ingawa hayanipendelei, Esther M Passaris ameshinda, tunastahili kumuunga mkono na kumwombea anapoendesha afisi ya mwakilishi wa kike bungeni kwa miaka mitano ijayo” ndiyo baadhi ya maneno ya Omanga.

Also Read
Kiwango cha maambukizi ya COVID-19 chashuka hadi asilimia 8.8

Alisema kwamba ataendelea kutagusana na watu wa Nairobi, kuwasaidia na kufanya kazi katika wadhifa tofauti.

Also Read
Serikali yajizatiti kukabiliana na visa vya moto Gikomba

Katika uchaguzi mkuu uliofanyika Jumanne tarehe 9 mwezi Agosti mwaka huu wa 2022, Esther Passaris wa chama cha ODM alijizolea kura 698,929 naye Millicent Omanga wa UDA akapata kura 586,246.

  

Latest posts

EACC kutwaa Mali ya shilingi Milioni 216 ya afisa mmoja wa kampuni ya KETRACO

Tom Mathinji

Gavana Waiguru awaalika Wawekezaji katika Kaunti ya Kirinyaga

Tom Mathinji

Maafisa wa Utawala waonywa dhidi ya kujihusisha na siasa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi