Mipaka ya Ghana kuendelea kufungwa ili kudhibiti msambao wa COVID-19

Mipaka ya Ghana ya ardhini iliyofungwa mwezi Machi mwaka 2020, itasalia kufungwa hadi wakati usiojulikana ili kuzuia uwezekano wa chamko la nne la maambukizi ya Covid-19 nchini humo.

Rais Nana Akufo-Addo,akilihutubia taifa,alisema serikali inaendelea kufuatlia na kuwa angalifu kuhusu athari ya ugonjwa huo na hata zoezi la kutolewa chanjo linaloendelea katika mataifa jirani kabla ya kufungua mipaka hiyo.

Also Read
FOCAC yanyanyua wakulima wa Afrika kimapato na kuondokana na umasikini

Wakati huo huo, huduma ya matibabu nchini Ghana (GHS) inasema shehena kubwa ya chanjo za Covid-19 zilizosambazwa kusini mashariki mwa eneo la Volta muda wake wa matumizi umekamilika kwa sababu ya ati-ati ma kujikokota kwa wanainchi kuchanjwa.

Also Read
Aliyekuwa Mama Taifa wa Malawi Ann Muluzi amefariki
Also Read
Madaktari waibua wasi wasi kuhusu kufurika kwa wodi za wagonjwa mahututi

Wakazi wa miji iliyoko mipakani wamelalamikia kufungwa kwa mipaka ya Ghana kwa muda mrefu,hatua iliyotekelezwa pindi janga hilo lilipochamka mwaka 2020.

Ni malori tu ya mizigo yanayoruhusiwa kuvuka kwenye mipaka hiyo iliyofungwa.

  

Latest posts

Boro wamtimua meneja Chris Wilder kwa matokeo duni

Dismas Otuke

Marekani kutatua mzozo wa mpakani baina ya Israel na Lebanon

Tom Mathinji

Aliyekuwa kiongozi wa kijeshi Burkina Faso Paul-Henri Damiba ajiuzulu

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi