Mitihani ya majaribio kwa darasa la nane na kidato cha nne kuanza Jumatano

Baraza la kitaifa la mitihani nchini-KNEC Jumatano linatarajiwa kuanzisha mitihani ya majaribio kwa wanafunzi wa gredi ya nne na darasa la nane.

Mitihani hiyo inatarajiwa kuendelea hadi siku ya jumatatu tarehe  26 mwezi Oktoba.

Also Read
TSC: Hatujafutilia mbali shughuli ya uajiri wa Walimu

Baraza hilo liliahirisha mitihani hiyo ambayo ilitarajiwa kuanza siku ya jumatatu kutoka na hafla ya sherehe za mashujaa ambazo ziliadhimishwa katika kaunti ya  Kisii.

Also Read
TSC: Walimu wengi hawajachanjwa dhidi ya Covid-19

Mitihani hiyo inalenga kutathmini uwezo wa wanafunzi wa kukumbuka kile ambacho wamejifunza na kuwawezesha kuangazia masomo baada ya kuwa nje kwa miezi saba kutokana na athari za janga la virusi vya corona.

Also Read
Huduma za afya kaunti ya Homa Bay zasitishwa kufuatia mgomo wa wahudumu wa afya

Wizara ya elimu haijatangaza tarehe za kufunguliwa kwa madarasa mengine swala ambalo waziri wa elimu George Magoha alisema litategemea hali ya virusi vya corona nchini.

  

Latest posts

Rashid Aman: Chanjo zinazotolewa hapa nchini ni salama

Tom Mathinji

Kampuni ya sukari ya Nzoia yalaumiwa kwa kutowalipa wakulima

Tom Mathinji

China kupiga jeki uwezo wa kuzalisha chanjo hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi