Mjane wa Waititu na wengine 12 wamezea mate kiti cha ubunge wa Juja

Kampeni za uchaguzi mdogo wa Eneo Bunge la Juja katika Kaunti ya Kiambu zimeanza huku kinyang’anyiro hicho kikiwavutia wawaniaji 13.

Kiti hicho kilibaki wazi kufuatia kifo cha Francis Munyua Waititu, aliyetambulika kwa jina maarufu la Wakapee.

Wagombea hao 13 tayari wameanza harakati za kuwania kiti hicho wakiwemo mjane wa Waititu Susan Njeri Waititu na George Koimburi aliyeshindwa na Waititu wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.

Also Read
Shughuli za Kampeini zasitishwa katika maeneo bunge ya Bonchari na Juja

Wawaniaji wengine ni pamoja na muwaniaji huru James Marungo na Eunice Wanjiru wa chama cha United Democratic Alliance.

Wakiongea na wanahabari baada ya kuwasilisha karatasi zao za uteuzi kwenye makao makuu ya chama cha Jubilee, Njeri na Koimburi walieleza imani kwamba chama hicho kitahifadhi kiti hicho.

Also Read
KRA yaboresha mfumo wake wa ukusanyaji ushuru

Walisema ajenda muhimu ni kukabiliana na ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana. Uchaguzi huo mdogo utaandaliwa tarehe 18 mwezi Mei.

Also Read
Majasusi wanamsaka afisa wa polisi mwanamke kwa kuwaua watu wawili

Chaguzi nyingine ndogo zitakazoandaliwa tarehe hiyo ni pamoja na uchaguzi wa Seneta wa Kaunti ya Garissa, Mbunge wa Bonchari na ule wa Mwakilishi Wadi ya Rurii katika Kaunti ya Nyandarua.

  

Latest posts

ODM yashutumu vikali ghasia za Migori dhidi ya Jimi Wanjigi

Tom Mathinji

Prof. Magoha: Mtaala mpya wa elimu hautatupiliwa mbali

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 795,600 aina ya Pfizer kutoka Marekani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi