Mjane wa Wakapee kupeperusha bendera ya Jubilee kwenye uchaguzi mdogo wa Juja

Mjane wa aliyekuwa Mbunge wa Juja Francis Munyua almaarufu Wakapee, Susan Njeri Waititu, anatarajiwa kuwania kiti cha ubunge cha Juja kwa tiketi ya chama cha Jubilee.

Njeri aliibuka mshindi kwenye uchaguzi wa chama hicho baada ya kupata kura 1,596 ikilinganishwa na mpinzani wake wa karibu Joseph Ng’ang’a aliyefanikiwa kupata kura 889.

Naftaly Rugara, ambaye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta (JKUAT) aliibuka wa tatu kwa kura 669.

Also Read
Mudavadi ajitosa rasmi ulingoni huku mwangwi wa BBI ukivuma kote nchini

Wengine waliokuwa wakiwania uteuzi wa chama cha Jubilee katika uchaguzi huo mdogo unaotarajiwa kuandaliwa mwezi Mei ni mfanyibiashara Antony Kirori na Karanja Ngarachu.

Uchaguzi huo wa chama cha Jubilee ulishuhudia idadi ndogo ya wapigaji kura, madai ya utoaji hongo, kukosekana kwa majina ya baadhi ya wapigaji kura kwenye sajili ya chama na madai ya kuhangaishwa kwa wasimamizi wa uchaguzi huo.

Also Read
Wafanyibiashara wa Soko la Mung’etho huko Kiambu walalamikia unyakuzi wa ardhi ya soko lao
Also Read
Serikali itatumia shilingi bilioni moja kufufua sekta ya Pareto nchini

Njeri aliahidi kushirikiana na wagombezi wote ili kukiwezesha chama hicho tawala kudumisha kiti hicho kilichoachwa wazi kufuatia kifo cha Francis Munyua aliyejulikana kwa jina jingine Wakapee.

Aliahidi kukamilisha miradi yote iliyoanzishwa na mumewe.

  

Latest posts

Justin Muturi kuwania urais kwa tiketi ya chama cha DP

Tom Mathinji

Bunge lapendekeza kuchunguzwa kwa mfumo wa ununuzi wa KEMSA

Tom Mathinji

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi