Klabu ya Gor Mahia imemteua Mjerumani Andreas Speir kuwa kocha mpya kumrithi Miwingereza Mark Harrison aliyetimuliwa wiki iliyopita.
Spier ana tajriba pana ya kufanya kazi ukanda wa Afrika Mashariki baada ya kuwaongoza APR ya Rwanda kunyakua ubingwa wa ligi kuu na kombe la shirikisho msimu wa mwaka 2013-2014,na pia
amehudumu kama mkurugenzi mkuu wa kiufundi wa shirikisho akiwa na timu timu za taifa za chipukizi ,na baadae kuhudumu katika nafasi ya mkurugenzi wa kiufundi katika shirikisho la kandanda nchini Rwanda .
Kocha huyo ana leseni ya ukufunzi ya UEFA Pro na atasaidiwa na kocha wa zamani wa timu taifa ya Kenya kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 17 , Michael Nam ambaye awali amekuwa katika timu za Homegrown FC, Agro-Chemicals, , Talanta na Vipers FC ya Uganda aliyoshinda nayo ligi kuu , kabla ya kuelekea Altabara ya Sudan Kusini mwaka 2021.